Happy kupata mtoto kwamtoa chozi
Na Imelda Mtema
Msanii wa kitambo katika tasnia ya filamu Bongo, Happy Nyatawe alikuwa akimuomba Mungu amjalie nafasi ya kuitwa mama bila mafanikio lakini hivi karibuni maombi yake yamejibu baada ya kupata mtoto wa kiume.Akizungumza na Ijumaa huku akitoa machozi ya furaha, Happy alisema amekuwa akiomba na kufunga atimize ndoto hiyo hivyo Mungu amesikia kilio chake.
“Jamani mimi nime muona Mungu sana, nyie ni mashahidi, leo hii na mimi naitwa mama, furaha niliyo nayo siwezi kuielezea,” alisema Happy.