The House of Favourite Newspapers

Joanita asherehekea bethidei kwa ‘kiyepe’ yai

0

Joanitacut561Na Hamida HASSAN

Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Makame ‘Joanita’ juzi ilikuwa siku yake ya kuzaliwa lakini cha kushangaza alisherehekea kwa kununua chipsi na mayai kisha kula na wasanii wenzake.

Jaonita alizaliwa Machi 1, mwaka ukiwa ni siri yake na ilipofika siku hiyo alikuwa lokesheni maeneo ya Kigamboni jijini Dar, alichokifanya mida ya lanchi alinunua chipsi zake na wasanii wenzake kisha akawataka wamuimbie kale kawimbo ka ‘hepi besidei tu yuuu’.

Akizungumzia tukio hilo, Joanita alisema: “Huwa sina makuu, nilichofanya kinatosha na wala sitafanya pati ya kufuru jamani.”

Leave A Reply