The House of Favourite Newspapers

Harmo Aja na Balaa Lingine!

0

DAR: Rais wa Lebo ya Konde Music Worldwide, Rajab Abdul ‘Harmonize’ ametangaza balaa jipya mwezi ujao wa Agosti.

Harmonize au Harmo, amesema yupo mbioni kusaini wasanii wake wapya watatu.

Kupitia Insta Story ya ukurasa wake wa Instagram, Harmo amesema kuwa, mashabiki wake watarajie mambo makubwa ikiwemo utambulisho wa wasanii wapya kwenye lebo yake.

“Dream team, three new artsts on August. It’s going to be fun..!” amesema Harmo au Konde Boy.

Kwa sasa lebo hiyo ina wanamuziki wawili; Harmo mwenyewe na kijana wake, Ibrah ambaye alisajiliwa mwezi Machi, mwaka huu na sasa anapasua anga.

Lebo hiyo inatajwa kuwa miongoni mwa lebo zitakazokuwa kubwa mno kwenye siku zijazo ndani na nje ya Bongo kiasi cha kuitisha lebo nyingine ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Akiwa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wiki iliyopita, Harmo alimshukuru Diamond au Mondi mbele ya Rais Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ kwa kumfungulia njia kabla ya mwishoni mwa mwaka jana wawili hao kutengana baada ya Harmo kujitoa Wasafi.

Chini ya Konde Boy Worldwide, Harmo amefanikiwa mambo mengi ndani ya mwaka mmoja kama kuachia ngoma mfululizo na Albam ya Afro East inayoendelea kufanya ‘wandaz’ sokoni.

Mbali na kuachia albam hiyo, pia amefanikiwa kumsaini msanii wake, Ibrah ambaye naye amekuwa ni moto wa kuotea mbali.

Stori: Happyness Masunga,Ijumaa

Leave A Reply