The House of Favourite Newspapers

Harmonize Atamani Kuwa na Mrembo Huyu

0

STAR wa Bongo Fleva, Rajab Abdul almaarufu Harmonize Konde Boy Mjeshi, ameendelea kusisitiza kuwa anahitaji mrembo wa aina flani ambaye atakuwa anashea naye bata ndani ya mjengo anaoishi wa kifahari alioupa jina la Konde Village ulipo Mbezi-Salasala jijini Dar.


Harmonize au Harmo
ameendelea kuposti video mbalimbali zikimuonesha akila bata ndani ya mjengo huo akimuomba mrembo yeyote ajitokeze ili awe naye kwenye uhusiano kwa ajili ya kuinjoi maisha pamoja kwenye mjengo huo wa kifahari wa ghorofa moja.


UAZLENDO WAMSHINDA

Mara baada ya kuachana
na aliyekuwa mpenzi wake ambaye ni mwigizaji wa Bongo Movies, Kajala Masanja ambaye walidumu takriban miezi mitatu, Harmonize au Konde Boy alitangaza kuwa yupo singo na ataendelea kuwa hivyo maisha yake yote, lakini sasa hivi uzalendo unaelekea kumshinda hivyo anahitaji mwenza kwenye maisha yake.

 

Moja ya video hizo ni ile iliyomuonesha akipasha kiporo cha chakula jikoni ambapo alieleza shauku yake ya kupata mwanamke ambaye atakuwa na sifa ya kujua kupika kama ilivyokuwa kwa Kajala.

 

Vyanzo vya ndani vinadai kwamba, wakati akiwa na Kajala, mkali huyo wa Ngoma ya Anajikosha alijikuta akinenepa kutokana na madikodiko aliyokuwa akipikiwa na mwanamama huyo mtaalam wa jiko hivyo anatamani kupata mrembo mwenye sifa kama hizo.

 

MWANAMKE MZURI

Kupitia Insta Story yake, Harmonize anasema; “Kitu pekee ninachomisi ni mwanamke mzuri ndani ya Konde Village…”Ni kweli kwamba, mjengo huo ni mkubwa mno kiasi kwamba, lazima mtu uwe mpweke kama utakuwa unaishi peke yako ndani yake.

Kabla ya kuwa na kajala, Harmonize alipita kwa mwigizaji Jacqueline Wolper kisha akafunga ndoa na Sarah ambayo ilivunjika baada ya kuwepo kwa tuhuma kwamba anatoka kimapenzi na video vixen wa wimbo wake wa Birdroom aitwaye Nicole.

 


ARUDI KWA SARAH?

Pia baada ya kuachana na
Kajala, Harmonize aliwaomba mashabiki wake wamsaidie majibu kwamba arudi kwa mkewe Sarah au uchagani kwa Wolper.

 

Hata hivyo, wengi walimshauri kwamba, ni heri akarudi kwa mkewe Sarah kwani Wolper tayari ana mtu wake ambaye amezaa naye na sasa amemchumbia ambaye ni Rich Mitindo.Harmonize ana mtoto mmoja wa kike ambaye amezaa na Mama Zuu ambaye naye kwa sasa ameolewa na mtu mwingine.

 


KONDE GANG RADIO NA TV

Wakati huohuo, Harmo
ametangaza kukamilika kwa vituo vyake vya redio na televisheni vinavyoitwa Konde Gang Radio na Konde Gang TV Kupitia Insta Story yake, Harmonize amesema tayari vitu hivyo vimekamilika kwa asilimia 100.Hata hivyo hakueleza kama vituo hivyo vitakuwa Dar au nyumbani kwao, Mtwara.

 

Harmonize anakuwa msanii wa pili kumiliki vyombo vya habari vya redio na televisheni baada ya bosi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye anamiliki Wasafi Radio na Wasafi TV.

STORI; MWANDISHI WETU

Leave A Reply