The House of Favourite Newspapers

Harmonize Kama Diamond Tu! Wachambuzi wa muziki Wafunguka Utunzi wa Mashairi

0
Msanii wa miondoko ya Bongo Fleva Harmonize ‘Harmo’.

MSANII wa miondoko ya Bongo Fleva Harmonize ‘Harmo’, anabaki kuwa mmoja wa wanamuziki bora kwa utunzi wa mashairi na ni bora kwa melodi na kwenye kugeuza matukio kuwa nyimbo. Huyu ni mtunzi mzuri.

Wachambuzi wa muziki wa kizazi kipya wanasema ni vigumu kutemana na Diamond Platnumz ‘Mondi’ kisha ukaendelea kukimbiza kimuziki, lakini Harmo ameweza.

Ni ukweli kwamba waliopishana na Mondi kwenye mitikasi ya muziki waliyumba ama kutoweka katika muziki huo.

Kwa Mondi kuna magwiji waongoza njia ambao ni Said Fela, Babu Tale na Salaam (SK).

Hawa wote wana mizizi mirefu ya muziki kwa sasa kiasi kwamba ukiwavimbia ujue una kesi kubwa.

Zamani ‘gemu’ lilizunguka eneo dogo tu la Kariakoo kwa Wahindi na vipindi vya burudani kwenye redio chache zilizokuwepo, leo hii muziki umeenda mbali zaidi na kwa sasa ukikosa ‘koneksheni’ umeisha.

Unaweza kufanyiwa umafia baadaye ukashangaa.

Diamond Platnumz ‘Mondi’.

Unaweza kupata dili za ‘kolabo’ na wasanii wakubwa  na taasisi kubwa za binafsi na Serikali, ukaula.

Harmonize amepitia huko kote kwani alikumbana na watu wenye pesa na ‘koneksheni’ kubwa ndani na nje ya nchi.

Lakini anaendelea, cha kufurahisha ni kwamba anaendelea kukimbiza mitaa na kwenye mitandao ya kijamii.

Ukitaka kujua nini unaambulia ukiachana na Mondi, muulize Rich Mavoko alipo sasa kabla ya kumchukulia poa Konde Boy.

Konde sasa hivi yupo daraja la juu ukiondoa Mondi na King Kiba, amewaacha wasanii wengi kimuziki na mafanikio.

Harmo hayupo pale kwa bahati mbaya, amefika hapo kutokana na mapambano na kuelewa njia ya kupita licha ya barabara kuwa na mabonde ya kila aina.

Konde huyu wa sasa ameshikamana na waliomshika mkono toka awali. Wanaomjua kindakindaki na wenye kuelewa nguvu na udhaifu wake, ina maana yupo vitani.

Hii ni vita ambayo kama hujajipanga  ni lazima utolewe kwenye reli.

Konde alikuwa kijana pendwa pale WCB lebo ya bwana mkubwa Diamond ambayo unaweza kusema ndiyo iliyomnoa makucha ya kisanii.

Harmo alijiunza kwa bidii kila kitu katika muziki wake kuanzia staili mpaka pozi kwenye video zake.

Kfupi aliamua kupita njia za bosi wake Mondi kwa kila kitu na wala hakujali maneno ya watu waliokuwa wakisema … ohoo anaiga.

Hakujali. Aliiga mpaka kuchukua mademu kwani aliwahi kujitwisha totozi saizi kubwa kuliko yeye kama Wolper, hii ilikuwa staili ya njia za Mondi ambaye alim’mbeba Zari mwenye umri mkubwa kuliko yeye.

Wapo waliomponda Harmo kwa tabia yake ya kumuiga Mondi. Kwamba kivuli cha Mondi kitamfanya awe chini kila siku.

Wakataka ajitafutie njia yake mwenyewe ya kuukuza muziki wake na aache kukopi na kupesti mambo au staili ya Diamond katika kukuza muziki wake.

 

Walisema hivyo kwa kuwa mashabiki wake, mashabiki wa Wolper na WCB, wote akawafanya ni timu yake na kubeba ukubwa pale WCB baada ya Mondi.

Alipotangaza kutemana na WCB wengi hawakuamini kama ni kweli.

Walijua ni ‘kiki’ kama ilivyo kawaida ya WCB. Mashabiki wengine wakasema Diamond anatafuta mtu wa kumshindanisha na Kiba badala ya yeye, ili ampoteze.

Walipoona ni jambo la kweli; stori zile zikabadilika.

Wale wale walioamini ni ‘kiki’, ndiyo walewale walioanza kudai kuwa Konde Boy atapotea kisanii kwa kujitoa WCB.

Hakuna aliyeamini kama Konde Boy anaweza kujiendesha nje ya WCB, ilionekana kama kinda asiyekuwa na mbawa za kumuwezesha kuruka peke yake.

Sasa hivi Konde amewahakikishia wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva kwamba ameweza kufanya kazi  nje ya WCB.

Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanasema bado ana mambo ya ki-WCB.

Ana muziki, sauti na melodi tamu. Lakini kila kitu anakisafirisha kupitia ‘kiki’ za mademu kama Diamond Platnumz ambaye ni bingwa wa kiki za matukio ya mapenzi.

Amewahi kutikisa kwa kiki ya mapenzi ya Wema Sepetu, Zari, Mobeto, Tanasha Donnah na wengine kibao.

Harmo naye kiki zake za  kimapenzi ni nyingi, hata ukizama kwenye ukurasa wa Konde pale Instagram, kinachokosekana ni jina Konde Gang tu.

Lakini mengine yote ni yaleyale ya WCB.

 

Harmo ni kama anadumisha ufalme wa WCB ama bila kujua au kwa kujua, ila kwa kuwa kukopi kunamlipa acha atusue kwa kuiga sauti, staili za kucheza na kiki.

Na Elvan Stambuli

#EXCLUSIVE: BABY MADAHA AFUNGUKA KUFUNGA NDOA NA ‘PASTOR’ – ”SIKUPANGA KUOLEWA”…

Leave A Reply