Video: Haya Ndiyo Maisha Halisi ya Harmorapa na Mpenzi Wake

Harmorapa akiwa kapumzika home kwake

Na IMELDA MTEMA|RISASI JUMAMOSI| MPAKA HOME

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa kijiwe hiki Mpaka Home, kama ilivyo ada ni kuwatembelea mastaa wa fani mbalimbali hapa Bongo na kuweza kuyajua maisha yao halisi ya kila siku nje ya kazi zao, wiki hii tulikuwa maeneo ya Mikocheni B nyumbani anapoishi kijana Athuman Omary wengi wakimfahamu kwa jina la Harmorapa.

TAZAMA VIDEO

Mahaba niue akimsaidia mpenzi wake kazi ya kufua.

Msanii huyo awali alikuwa akiishi Vingunguti jijini Dar, lakini sasa maisha yamebadilika kidogo, ameweza kupata  nyumba kubwa maeneo ya Mikocheni  na hiyo yote ni kutokana na sapoti kubwa anayopewa na bosi wake aitwaye Irene Sebuka.

  

Nyumbani hapo msanii huyo ambaye anafanana na mkali wa kutoka Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Harmonize, anaishi na mwanamke wake aitwaye Nancy au anavyopenda kumuita mwenyewe Wolper, wake.

Ungana nami hapa chini ili uweze kujua anaishije nyumbani hapo.

…akiandaa kitoweo na mpenzi wake

 

Kwanza ilikuwaje mpaka akajiita Harmorapa?

“Unajua hata wewe mwenyewe ukiniona hakuna ubishi kwamba mimi sifanani na Harmonize sasa kwa vile naimba na nikaona wazi niko kama yeye ndio maana nilijipa jina hilo na nilikuwa natamani sana nimuone na yeye anione mimi pacha wake.

…akimnywesha soda

Nini kimebadilika kwenye muziki wake kati ya zamani na sasa?

“Maisha yapo tofauti sana kwa kweli sasa hivi, nyuma nilikuwa sina muelekeo na chochote lakini sasa hivi maisha yangu nayaona kabisa katika mwanga ulio bora kabisa na ninajivunia kuwa mimi siku zote  na hata hivyo zamani nilikuwa naishi Vingunguti lakini sasa Mikocheni tofauti kubwa sana.

Zamani alikuwa akifanya kazi gani zaidi ya muziki? 

Zamani nilikuwa nauza mabegi ya kike na ya kusafirisha hadi Mwenge kuuza, ndio ilikuwa ni biashara kubwa japokuwa nilikuwa na ndoto ya kuwa mwanamuziki  lakini nilijua wazi ipo siku Mungu angesikia kilio change.

Wolper wake ameshamuoa? Anaishi naye?

“Huyu bado sijamuoa lakini ninaishi naye na si unajua Kibongobongo ukikaa na msichana ndio mke kabisa, basi tuombe Mungu mambo yatakuwa mazuri kabisa huko mbeleni.

…chakula kikiandaliwa

Alimpataje mpenzi wake? Haogopi kuibiwa?

“Huyu alikuwa ni mteja wangu wa mapochi Mwenge, kwa hiyo nikamzoea tukazoeana mpaka ikatokea hivyo na tuna mwaka sasa na kuhusu kuibiwa hiyo ni akili yake kwa maana akiamua kufanya hivyo atakuwa ni yeye mwenyewe lakini mimi sina wasiwasi naye.

Ni kitu gani anapenda kufanya akiwa nyumbani?

“Mara nyingi mimi nikiwa na mapumziko nyumbani napenda sana kufanya usafi na muda mwingi kufua nguo na hata kumfulia mpenzi  wangu. Baada ya hapo ni kuangalia TV hususan wanamuziki mbalimbali wa nje.

Harmorapa akiwa na meneja wake.

Mafanikio aliyonayo yanatokana na muziki au kitu kingine?

Japokuwa ninaimba muziki lakini nashukuru Mungu, bosi wangu Irene Sabuka, ameniajiri katika kampuni yake ya kuuza vifaa vya magari Kariakoo na ndipo huko maisha yangu yalipobadilika  hivyo sitegemei muziki tu.            

…akimwagilia maua.

Ni chakula gani anapenda? Vipi kuhusu mavazi?

“Sifa moja kubwa ya mpenzi wangu ni kujua kunipikia mchele wa Pisholi na nyama. Kuhusu mavazi, mimi napenda sana kupendeza yaani nikitinga tisheti na jinzi naona niko freshi na nguo ambazo wanapenda kuvaa mabraza meni.

Maisha gani alipitia huko nyuma?

“Nyuma sitaki kukumbuka kabisa, nilipitia maisha mabaya sana na ya dhiki mno. Sitaki kurudi huko nyuma nilikotoka na ninaomba Mungu anisaidie kwa hilo.”

Save

Save

Save

Save

Save

Toa comment