The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Anjella wa Harmonize Apelekwa Mjini

0

MSANII wa Bongo Fleva, Harmonize, amesherehekea siku ya Valentines kwa kuachia ngoma yake mpya #AllNight aliyomshirikisha msanii chipukizi, Anjella.

 

 

Harmonize ametimiza ahadi yake kwa Anjella kuwa atampeleka mjini, mara tu baada ya kuona clip zake akiimba na kuvutiwa na kipaji chake.

 

 

Katika ngoma hiyo Anjella ameimba chorus na lugha iliyotumika kwa kiasi kikubwa ni Kiingereza. Kwa mujibu wa Harmonize, hii ndiyo single yake ya kwanza official kuitoa kwa mwaka 2021.

 

 

Harmonize ameanza na audio na huenda akaachia video ya ngoma hiyo muda si mrefu, kwani tayari alishadokeza kuwa ipo tayari muda mrefu.

Leave A Reply