The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Mwanafunzi Aliyepotea Mbeya Apatikana

0

Mwanafunzi Ester Noah Mwanyiru aliyepotea kwa muda wa siku 20 tangu asubuhi ya tarehe 18 Mei 2023 hatimaye amepatikana ndani ya masaa 24 tangu agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoka akimwelekeza mkuu wa mkoa wa Iringa, Juma Homera pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa haraka kuhusiana na kupotea kwa binti huyo.

Ester, mwanafunzi aliyedaiwa kupotea Mbeya

 

 

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa maagizo hayo hapo jana (Alhamisi, Juni 22, 2023) baada ya kupokea clip yenye maelezo ya mzazi wa binti huyo ambaye alikuwa akisoma kidato cha tano, tahsusi ya PCB kwenye shule hiyo.

Waziri Mkuu Majaliwa akitzungumza jambo

 

Katika clip hiyo, Mama yake Esther anadai kwamba yeye na mume wake waliitwa na uongozi wa shule hiyo na kujulishwa kwamba Esther hajaonekana tangu asubuhi ya tarehe 18 Mei, 2023 na kwamba hadi sasa zimepita siku zaidi ya 20 wamekuwa wakimtafuta binti yao kila mahali lakini hakuna dalili za kumpata.

Mama Esther anadai kuwa Esther aliacha ujumbe wa maandishi akiwaaga rafiki zake na kuomba Mwalimu Jimmy aache kuwafanyia wanafunzi wengine kitendo alichomfayia yeye kwani kimesababisha maisha yake kuwa magumu.

 

 

“Naomba umfikishie salamu Mwalimu Jimmy, mwambie ameyafanya maisha yangu kuwa magumu sana hapa shuleni. Asiendelee kuwafanyia wanafunzi wengine kama alivyoyafanya maisha yangu mimi kuwa magumu,” alisema mama yake Esther akisoma sehemu ya ujumbe huo.

 

 

Hadi hivi sasa bado kuna mahojiano yanaendelea kati ya binti huyo na Jeshi la polisi ili aweze kukabidhiwa kwa mama yake na hatimaye kwenda nyumbani.

 

Leave A Reply