The House of Favourite Newspapers

Hawa Nd’o Makocha Wanaotajwa Kumrithi Kaze Yanga

0

IMEELEZWA kuwa miongoni mwa makocha ambao wanatajwa kubeba mikoba ya benchi la ufundi ndani ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kikinolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ni pamoja na Mecky Maxime.

 

 

Kaze na benchi lake la ufundi, jana Machi 7 walifungashiwa virago kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo kwa mujibu wa uongozi.

 

 

 

Timu hiyo mchezo wake wa mwisho kwa mzunguko wa pili kushinda ilikuwa mbele ya Mtibwa Sugar ambapo ubao Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-0 Mtibwa Sugar.

 

 

Kwa mujibu wa Yanga benchi la ufundi litatangazwa hivi karibuni kabla ya ligi kuendelea kushika kasi mzunguko wa pili.

 

 

 

Maxime ambaye amefutwa kazi ndani ya Kagera Sugar anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya viongozi ili kuweza kumpa kazi hiyo ya kuwanoa vinara hao wa ligi.

 

 

 

Mbali na Maxime pia Kocha Etienne Ndayiragije ambaye ‘alichimbishwa’ ndani ya timu ya taifa ya Tanzania  (Taifa Stars) jina lake pia linatajwa kuwa miongoni mwa makocha ambao wanaweza kurithi mikoba ya Kaze.

Leave A Reply