Hawa Wa Diamond Ana Hali Mbaya, Mama Yake Alia Kwa Uchungu – Video
Mama mzazi wa msanii wa muziki kipya, Hawa Nitarejea @hawanitarejea ameangua kilio mbele ya Global TV baada ya kuelezea kuwa mtoto wake huyo amekuwa akijifungia ndani kwa takribani miezi miwili sasa, akiwa hali chakula vizuri wala mtoto wake mdogo hampi chakula kama inavyotakiwa, kitu ambacho kinamchanganya sana na kumuumiza kupita kiasi.
Mama huyo alisema kuwa anaumia sana kwa sababu, wametoka kwenye janga zito sana la kuuguza ugonjwa uliokuwa ukimsumbua lakini sasa hivi limeibuka tatizo lingine la kujifungia ndani, kutokula vizuri na kutoongea na mtu yeyote pale zaidi ya mtoto wake pekee.
Mama huyo ameomba msaada kwa wanasaikolojia wanaoweza kuongea na mtoto wake kwani huenda ikawa ana stress za kutofanya kazi yake ya muziki muda mrefu.