The House of Favourite Newspapers

Hili la Kusagana, Mastaa Mnapaswa Kulikemea

0

binti (3)Malkia Said a.k.a Malkies, binti wa miaka 19 aliyefunguka kuwa ni msagaji.

KWENU mastaa wa kike Bongo, nawasalimu kwa umoja wenu maana mpo wengi, siwezi kuwataja mmojammoja  kwa majina.

Habarini za siku, vipi mnaendeleaje na mishemishe za kila siku? Maisha yanasemaje? Hongereni kwa kuwa mastaa, maana najua wapo wengi ambao wanatamani kuwa, lakini kwa namna moja au nyingine wameshindwa.

Mkitaka kujua afya yangu, mimi ndugu yenu sijambo. Namshukuru Mungu, naendelea kupambana katika eneo langu la kazi. Nawahabarisha na kuwaelimisha Watanzania kupitia magazeti Pendwa Bongo.

Nimewakumbuka leo mastaa wa kike kupitia barua nzito, nina jambo nataka kuwaeleza na tafadhali sana, lichukulieni suala hili kwa uzito wake.

Ndugu zangu, kwa muda mrefu nimekuwa nikielezwa suala la mastaa kusagana. Tetesi zimewataja mastaa wengi tu wa kike kwamba wanahusika katika mchezo huo. Najua mnajijua, sina sababu ya kutaja majina yenu.

Nililifanyia kazi tetesi hizo na kubaini kwamba zina asilimia nyingi ya ukweli ndani yake. Sababu kubwa iliyotajwa kusababisha wengi wenu muingie kwenye mapenzi hayo ya jinsia moja ni kutotaka usumbufu.

Kwamba wanaume wana usumbufu. Wanawatumia kwa wakati fulani kisha wanawamwaga. Sababu nyingine iliyotajwa ni kwamba mnafanya mchezo huo kwa sababu unawaepusha na magonjwa hatari kama Ukimwi na mengineyo.

Kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele, tatizo hilo linatajwa kushika kasi Bongo. Awali ilikuwa ni jambo la aibu na siri, lakini siku hizi linafanyika bila hofu.

Naambiwa kwamba wahusika mnawajua. Kuna wanawake ambao ndiYo mnawaita wanaume. Hivyo staa anaweza kuwa wa kike lakini anawashughulikia wenzake au staa anaweza kuwa anashughulikiwa na mwanamke mwingine ambaye anajifanya mwanaume.

Wiki iliyopita kupitia gazeti ‘dugu’ na hili la Risasi Jumamosi, tuliona mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Malkia, akielezea kwa kirefu uzito wa tatizo hili. Akaenda mbali kwa kusema alikuwa amnase mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ lakini ikashindikana licha ya kuwa tayari alishamrushia ‘ndoano’ za kutosha.

Ndugu zangu hapa inatupasa kidogo tumuogope Mungu. Hili ni tatizo, hakuna sababu ya kulifumbia macho. Mnaofanya hivyo mjue kwamba huu si utamaduni wetu. Mambo hayo yamekuwa yakifanywa huko ughaibuni.

Sidhani kama una manufaa kwetu. Sanasana tunaharibu maadili na kizazi kijacho. Wanaoshiriki wabadilike, wafuate utaratibu wa halali ambao ndio unafahamika hata katika maandiko ya dini.

Kwamba mwanaume atatembea na mwanamke na wawili hao watapata mtoto. Uhusiano wa mwanamke kwa mwanamke tunautoa wapi? Una faida gani katika jamii yetu?

Ni vyema tukachagua, kuishi katika maadili yetu ya Kitanzania. Tukaachana na masuala ya kuiga ambayo hayaleti picha nzuri katika jamii inayotuzunguka.

Wote mnaofanya vitendo hivyo mnajijua, kila mmoja achukue hatua. Aache kabisa tabia hiyo kwani hata sababu zinazowafanya muingie huko hazina mashiko, mnajidhalilisha.

Ni matumaini yangu mtakuwa mmenielewa na mtabadilika kitabia.

Mimi ni kaka yenu;

Semina Kubwa ya Eric Shigongo Ilivyowafungua Akili Vijana: Part 1

Semina ya Eric Shigongo Iliyowainua Vijana Kiuchumi, Part 2

Leave A Reply