Hitilafu ndani ya kizazi “Endometriosis”

Blausen_0349_EndometriosisKizazi au mfuko wa kizazi una tabaka tatu, kwanza ni tabaka la ndani kabisa linaitwa ‘Endometrium’. Tabaka hili ni ngozi laini sana, hutoka na kuota nyingine pale mwanamke anapopata damu ya hedhi.

Pia mimba inapoharibika au kusafisha kizazi, tabaka hili husaidia kutunza na kulea mimba.

Tabaka la pili ni lile la kati linaitwa ‘Myometrium’, hili limetengenezwa kwa misuli imara ya kizazi ambayo hufunika na kusinyaa. Misuli hufunika wakati wa ujauzito na husinyaa mara tu baada ya kujifungua, au unapokuwa na uvimbe, uvimbe ukishatolewa husinyaa. Misuli hii ina nyuzinyuzi zinazovutika.

Tabaka la tatu la kizazi ni la nje liitwalo ‘Perimetrium’ au ‘Serosa’ ambalo limegusana na viungo jirani kama utumbo, kibofu cha mkojo na mfuko wa haja kubwa.

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Tunaposema ‘Endometriosis’ ni kwamba huu ni ugonjwa ambao katika hali isiyo ya kawaida lile tabaka la ndani la kizazi ‘Endometrium’ badala ya kuota kwa ndani, huota kwa nje.

Tumeona katika tatizo la kuvimba kwa kizazi ‘Adenomyosis’ hili tabaka la ndani huota katika tabaka la kati, lakini hapa tabaka hili huota nje ya kizazi.

Chanzo cha tatizo hili bado hakijulikani lakini vipo viashiria vya tatizo hili mfano kuwa na historia ya tatizo hili katika familia, kama yupo ndugu wa karibu aliyewahi kulipata.
Tatizo hili hushambulia vifuko vya mayai, mirija ya uzazi na viungo vyote jirani na kizazi. Mara chache sana tatizo hili husambaa mbali kutoka katika eneo la kizazi.

Tatizo hili la ‘Endometriosis’ husababisha kila mwezi litoe damu kama ilivyo katika mzunguko wa hedhi, kwa hiyo uwepo wake nje ya kizazi linapo’bleed’ husababisha majeraha kutokana na hali iitwayo ‘Inflammation’.

Majeraha huwa na tabia ya kupona yenyewe hivyo kutengeneza makovu na hali ya kushikamana. Hali hii inapoendelea husababisha matatizo makubwa tumboni katika viungo vyote jirani.

DALILI ZA UGONJWA
Mgonjwa hulalamika maumivu ya tumbo upande wa chini kuzunguka kiuno kwa ndani zaidi, kutoshika kwa zaidi ya mwaka mmoja, maumivu haya ya chini ya tumbo kuzunguka kiuno huwa sugu, hupata nafuu akitumia dawa lakini baadaye hujirudia.

‘Chronic pelvic pains’ maumivu huwa kila siku lakini unapokuwa katika siku zako huwa makali zaidi. Vilevile mgonjwa hupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa. Maumivu haya hutokea wakati na baada ya tendo. Wanawake wengi wenye tatizo hili huishia kuwa wagumba.

Mara chache tatizo hili huambatana na matatizo katika mfumo wa mkojo au haja kubwa.
Itaendelea wiki ijayo.


Loading...

Toa comment