The House of Favourite Newspapers

Hongera Serengeti Lite, Wengine Jitokezeni

LIGI Kuu ya Wanawake Bara ‘Serengeti Lite Premier League’ imeonekana kukubalika haraka kufuatia wadhamini ambao ni Serengeti Lite kujitokeza kusapoti ligi hiyo.

 

Hapo nyuma hakujawahi kuwa na ushindani mkubwa kama ilivyo msimu huu ambapo ligi hiyo imejikuta ikipata mashabiki viwanjani hususan jijini Dar.

Wikiendi iliyopita kwa mara ya kwanza derby ya Simba na Yanga kwa wanawake ilipigwa na mashabiki waliojitokeza walikuwa wengi, haya ni mafanikio makubwa sana kwenye ligi na Serengeti wametufanya tuione hiyo derby.

 

Championi tunawapongeza wadhamini wa ligi hiyo, Serengeti, kwa kujitolea tangu msimu uliopita kuidhamini ligi hii ambayo sasa itasaidia upatikanaji mzuri wa timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’.

 

Hapo mwanzo ilikuwa ngumu kupata kikosi cha timu ya taifa kwa wachezaji kutoka mikoani zaidi ya kuchukuliwa wale wa jijini Dar na mikoa michache ambako ligi ndogo zilikuwa zikichezwa lakini sasa wigo ni
mpana kwa kocha wa Twiga kuchagua vipaji kulingana na uhitaji wake.

Hivyo ni fursa kwa makampuni mengine kuiga walichofanya Serengeti Lite, ukiangalia awali kabla hawajaingia na kuwekeza kwenye ligi hii hali ilikuwa mbaya na wachezaji walicheza kwa kujifurahisha lakini sasa ushindani na kila timu inaweza kupata kombe na zawadi.

Utaona hata Simba Queens imesajili mchezaji kutoka nje ya nchi, haya ni mafanikio yaliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na wadhamini Serengeti wakishirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Ni vyema makampuni mengine nayo yakajitokeza kudhamini ligi nyingine kama daraja la kwanza na nyingine nyingi.
Nunua

Comments are closed.