Hukumu Kuhusu Bomoabomoa Kutolewa Kesho
Wakili wa mlalamikaji anayesikiliza kesi hiyo, Abubakar Salim, akihojiwa na wanahabari baada ya kutoa taarifa kwa wakazi waliobomolewa nyumba zao mabondeni waliokuwa wamejitokeza kusikiliza kesi ambayo maamuzi yake yatatolewa kesho.
Wananchi wakimsikiliza wakili Salim (hayuko pichani).Baadhi ya wananchi waliofika mahakamani hapo.
KESI ya kupinga bomoabomoa iliyotarajiwa kutolewa maamuzi leo jijini Dar es Salaam katika Mahakama Kuu kitengo cha ardhi imeahirishwa tena, badala yake hukumu itatolewa kesho.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulya, (CUF) ambayo inataka wananchi hao mbali na kubomolewa wapewe maeneo mbadala na yenye usalama ambapo wakili wa upande wa mlalamikaji akiwa ni Abubakar Salim aliyewataka wananchi waliokuwa nje ya mahakama hiyo kutochoka kuendelea kufuatilia kesi hiyo.
NA DENIS MTIMA/GPL