The House of Favourite Newspapers

Hushiki mimba? Soma hapa-2

0

pregnancy-test-120305Wiki iliyopita tulizungumzia kuhusu aina za uvimbe kwenye tezi za uzazi za mwanamke. Leo tunazitaja aina saba za uvimbe huo ambazo kitaalam zinaitwa Sisti.

1 .Sisti/Nziba inayopatikana kwenye Foliko (Follicular Cyst). Huu ni uvimbe ambao hutokea wakati Uovuleshaji (Ovulation) usipotokea au baada ya Kopasi Leteamu (Corpus Luteum) kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutopachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi.

Uvimbe huu unakuwa na wastani wa upana wa inchi 2.3. Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali katikati ya mzunguko wa hedhi, kwa maana ya siku ya Uovuleshaji (Ovulation). Maumivu haya huonekana kwa robo ya wanawake wenye aina hii ya uvimbe. Kwa kawaida, uvimbe huu hauna dalili zozote za wazi na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa.

2. Sisti/Nziba inayokuwa kwenye Kopasi Luteamu (Corpus Luteum Cyst). Huu ni uvimbe unaotokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi.

Kwa kawaida Corpus Luteum husinyaa na kupotea yenyewe, au wakati mwingine inaweza ikajaa maji, hivyo kusababisha uvimbe wa aina hii. Uvimbe huu huonekana kwenye upande mmoja (kushoto au kulia) wa mwanamke na hauna dalili zozote zile.

3. Sisti/Nziba yenye kutoa damu (Hemorrhagic Cyst). Huu ni uvimbe unaotokea              wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ule, ambao umeshajitengeneza tayari. Huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke (kushoto au kulia).

4. Sisti/Nziba ya Demoidi (Dermoid Cyst). Uvimbe huu ambao si saratani, hujulikana pia kama Teratoma kubwa yenye                            Sisti/Nziba (Mature Cystic Teratoma).

Aina hii huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika mimba, na huweza kukua na kufikia inchi sita (6) kwa upana na ndani yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mfupa, mafuta na gegedu (Cartilage).

Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa zaidi au kujizungusha, hivyo kuathiri usambazaji wa damu kwenda kwenye uvimbe huu na kwa hiyo kusababisha maumivu makali maeneo ya tumboni.

5. Sisti nyingi (Polycysitic appearing Cyst). Uvimbe wa aina hii unakuwa ni mkubwa                    sana, na huwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogo vidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.

6. Adenoma yenye Sisti (Cystadenoma). Hii ni aina ya uvimbe unaotoka kwenye tishu za Ovari na hujazwa na majimaji yenye kuvutika. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana.

7. Sisti kwenye Endometria (Endometriomas/Endometrial Cyst).

Uvimbe huu husababishwa na uwepo wa aina                         mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama Endometria (Endometrium) kwenye mayai ya mwanamke. Aina hii huathiri wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito na huambatana na maumivu sugu ya nyonga wakati wa hedhi. Uvimbe huu unakuwa na damu ya rangi nyekundu inayoelekea kuwa kahawia na ukubwa wake ni kuanzia inchi 0.75 hadi 0.8.

Ni nini chanzo cha uvimbe kwenye tezi za uzazi za mwanamke? Vihatarishi vikuu vya tatizo la uvimbe kwenye tezi za uzazi za mwanamke, kwanza ni historia ya awali ya Sisti/Nziba kwenye Ovari (Ovarian Cyst). Kwa kawaida, wanawake ambao wazazi wao au watu wao wa karibu wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo, wanakuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kupatwa na tatizo hilo.

Sababu nyingine inayoweza kusababisha uvimbe katika Ovari za mwanamke ni kuwa na mzunguko wa hedhi usiokuwa na mpangilio maalum au kama tunavyouita kwa kimombo, Irregular Menstruation Cycle. Kihatarishi kingine ni kuwa na mafuta mengi kwenye sehemu ya juu ya mwili. Tatizo hili mara nyingi linawapata wanawake wanene.

Ugumba na kuvunja ungo au kubalehe mapema, ni sababu nyingine. Mtoto wa kike anapobalehe akiwa na umri wa miaka kwa mfano 11 au chini ya hapo, huweza kupatwa na uvimbe katika Ovari zake. Aidha, kukosekana uwiano sawa wa vichocheo au homoni mwilini au ugonjwa wa Hypothyroidism na pia dawa ya kutibu saratani ya matiti ya Tamoxifen, husababisha tatizo hilo.

Leave A Reply