The House of Favourite Newspapers

Huyu ndiye ‘mchawi’ mafanikio ya Joh Makini

0

johm20akini20MIAKA ya mwanzoni mwa 1990, John Simon ‘Joh Makini’ akiwa kijana mdogo mwenye kiu ya siku moja kufanikiwa alikuwa anapenda sana kusoma vitabu vya kuelimisha ambapo moja ya vitu ambavyo hatavisahau alivyojifunza ni kwamba, mtu ili kufanikiwa maishani ni lazima uwe na sababu ya kutaka mafanikio ikiwa ni pamoja na kumchagua mtu ambaye amefanikiwa na kuzifuata nyayo zake.

Joh Makini anayeiwakilisha Arusha, amesema siku zote amekuwa akiamini hivyo kama alivyojifunza akiwa kijana mdogo na hajawahi kupuuza juu ya elimu hiyo iliyompa mwanga maishani kwake.

Amepambana huku moyoni akimfuata ‘mchawi’ wa mafanikio yake ambaye amemweka wazi katika makala haya. Amefunguka mengi ikiwemo ngoma yake mpya ya Perfect Combo pamoja na mambo mengine kuhusu muziki na maisha yake binafsi.

Tujiunge naye katika mahojiano na BMM (Burudani Mwanzo Mwisho).

BMM: Vipi mapokeo ya Perfect Combo sokoni?

Joh: Inafanya vizuri, namshukuru Mungu si kama ngoma zilizopita, hii imenifanya nipige hatua nyingine kwenye kazi yangu maana simu ni nyingi hasa kutoka nje ya nchi za watu wanaotaka tufanye kazi pamoja.

BMM: Unaweza kututajia baadhi yao?

Joh: Muda ukifika nitaweka wazi, kwa sasa bado niko kwenye mazungumzo nao.

BMM: Vipi una mpango wa kufanya ‘media tour’ hasa Nigeria kwa kuwa umefanya ngoma na msanii anayefanya vizuri zaidi huko?

Joh: Mipango kiukweli ipo, niweke wazi tu niko kwenye maandalizi na timu yangu na mambo yakiwa mazuri tutaelekea Nigeria kwa ajili ya kuipushi zaidi.

BMM: Baadhi ya mistari kwenye ngoma ya Perfect Combo imesikika kwenye kolabo uliyofanya na Chidimma kwenye msimu wa Coce Studio uliopita na hata mdundo kwa mbali ni kama uleule, huoni hilo linaweza kuwa limepunguza uzito fulani wa wimbo huu?

Joh: Sidhani kama hilo linaweza kuwa tatizo ilimradi tu mistari kwenye ngoma ile ya kwanza niliandika mimi mwenyewe. Hata hivyo, ukisikiliza vizuri utagundua tofauti ipo na mistari yenyewe siyo mingi ni michache tu kwenye ubeti wa pili.

BMM: Unaweza kueleza kibiashara imekaa vipi, Nikki wa Pili ambaye uko naye kwenye kampuni moja ametoa ngoma hivi karibuni (Sweet Mangi) wakati ambao ndiyo kwanza wimbo wako unapamba moto, hamuoni kwamba mnazimana wenyewe?

Joh: Hakuna tatizo lolote lile kibiashara man, muziki mzuri always unajiuza wenyewe, kazi zetu zote ziko vizuri so nafikiri ni muda muafaka wa mashabiki kufurahia muziki mzuri kutoka kwetu.

BMM: Mbali na kazi zako, unaweza kuwaeleza mashabiki nani hasa chachu ya mafanikio yako kimuziki, yaani unamsikiliza na kufuata nyayo zake.

Joh: Kiukweli ninawasikiliza watu wengi sana, yaani ukipanda kwenye gari langu unaweza kuchizika kwa ngoma ninazosikiliza, lakini mchawi anayenipa ‘insparation’ siku zote ni Dk Remmy Ongala. Aisee Huyu jamaa alikuwa ‘genius’, muziki wake unaishi siku zote, ninapomsikiliza napata nguvu ya kufanya kazi nzuri.

BMM: Wewe ni miongoni mwa wasanii wanaokwepa sana mambo yao ya uhusiano kuyaweka wazi. Kama hutajali, leo ‘exclussive’ hata kwa ufupi sana kuhusu uhusiano wako!

Joh: No siwezi kuzungumza lolote lile kuhusu uhusiano. Ninakutanishwa na mashabiki kwa sababu ya muziki tu basi!

BMM: Hili ni swali pengine unaulizwa kila mara lakini siku zote huwa majibu yake yanabaki yanazaa maswali mengine. Si vibaya nikauliza tena, kwa nini Lody Eyez na Bonta hawasikiki kwenye kazi za Weusi na mnadai kuwa ni wanakundi?

Joh: Weusi ni kampuni si ndiyo? Sasa kampuni ni mimi, Nikki, G Nako, Lody Eyes na Bonta, hao ndiyo watu tunaounda kampuni. So kama akisikika Nikki ina maana Weusi wamesikika, nikisikika mimi, Lody au G, tunakuwa tumesikika Weusi wote. So kutosikika kwa hao uliowataja sidhani kama nina majibu yao, wapo, watafute uwaulize.

BMM: Kwa kumalizia unawaambia nini mashabiki wako?

Joh: Wazidi kunisapoti, siwezi kuwaangusha.

Leave A Reply