The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mama wa Mtoto Aliyenusurika kwa Mabomu Akafariki kwa Ajali Karatu

0

KUFUATIA tukio la ajali mbaya iliyoondoka na roho za watu 35 miongoni mwao wakiwemo wanafunzi 32 wa Shule ya Lucky Vincent, walimu wawili na dereva mmoja, mama wa mtoto Anord Alex Swai ambaye pia alifariki kwenye ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita huko Karatu, ameeleza kwa masikitiko namna ambavyo aliagana na mwanaye mara ya mwisho.

Akizunguma na Global TV Online baada ya kuaga miili ya marehemu hao katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid juzi Jumatatu, Mama Agrippina Swai anasema;

“Mtoto wangu alinusurika kwenye tukio la mabomu kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi, Olasiti, tarehe 5 /5 /2013”

“Namshukuru Mungu amemtoa tena kipindi hiki wakati akienda kufanya mtihani na wenzake.

“Wazazi wenzetu Mtuombee, muiombee familia ya swai ambayo imeshindwa kuubeba huu msiba”

Mtoto Arnold alivyonusurika bomu mwaka 2013.

Alichoongea na mwanaye mara ya Mwisho

“Mara ya mwisho mimi nilikuwa nasafiri kwenda kijijini kuwaona wazazi ambao nao ni wagonjwa, akaniaga akaniambia mama ufike salama, akamuaga na dada yake ambaye alitakiwa kwenda kufanya interview leo, akamwambia dada nakuombea upate kazi” alisema Mama Swai huku akilia kwa uchungu.

MSIKILIZE HAPA AKIZUNGUMZA KWA UCHUNGU

Leave A Reply