The House of Favourite Newspapers

Ibenge Afunguka Dili la Kisinda Kutua Morocco

0

HATIMAYE Kocha wa RS Berkane ya nchini Morocco, Frolent Ibenge amefunguka juu ya dili la winga wa Yanga, Tuisila Kisinda kujiunga na klabu hiyo ambayo anaifundisha.

 

Ikumbukwe Ibenge ndiye kocha aliyemkuza winga huyo tangu akiwa na umri wa miaka 19 walipokuwa katika kikosi cha AS Vita ya nchini DR Congo.

 

 

Akizungumza na Championi Jumatano moja kwa moja kutoka nchini Morocco, Ibenge alisema kuwa amezisikia taarifa za winga huyo kuhusishwa kujiunga na timu yake na ni jambo zuri kwa kuwa Kisinda ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa.

 

“Nimesikia kuhusu Berkane kumuhitaji Kisinda, ni mchezaji mzuri ambaye namfahamu tangu hapo awali tukiwa wote AS Vita, sio mbaya sisi kuhusishwa naye, ila kwa sasa siwezi kuzungumza chochote kwa kuwa bado haijathibitishwa kuwa ni mchezaji wetu,” alisema kocha huyo.

Leave A Reply