The House of Favourite Newspapers

IGP Sirro Afanya Mabadiliko kwa Ma-RPC

0

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi, ambapo aliyekuwa RPC wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa, amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma na aliyekuwa RPC Morogoro, Wilbroad Mutafungw,a amekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Tanzania.

 

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa Desemba 3, 2020,  ambapo  Sirro amesema kuwa kwa sasa hali iko shwari na bado wanaendelea na oparesheni mbalimbali ikiwemo dawa za kulevya na matuko ya unyang’anyi.

 

Amesema hayo yamewezekana kutokana na ushirikiano uliopo kati ya vyombo vya usalama na wananchi wanaochukia uhalifu na wadau mbalimbali.

 

Aidha ametoa wito kwa Watanzania wote wenye mawazo chanya kwa nchi yao kushirikiana na vyombo vya usalama katika kubaini na kuzuia uhalifu.

 

Leave A Reply