The House of Favourite Newspapers

IGP Sirro Awafariji Wafiwa wa Viongozi Kibiti

0

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti alipokwenda kuwapa pole baada ya kupokea taarifa ya mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho usiku wa kuamkia jana.

Sirro amewata wananchi wa kijijini hapo kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.

Waliofariki katika tukio hilo ni Ofisa Mtendaji, Mwarami Shamte aliyekutwa na majereha matatu ya risasi na Mwenyekiti wa Kijiji, Hamis Bakari Mkima aliyekutwa na jeraha moja.

Pia wauaji hao walimpiga, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo, Michael Martin risasi ya macho, iliyoharibu macho yake mawili.

Kama hiyo haikutosha, waliichoma moto nyumba ya Martin na kisha kutokomea kusikojulikana.

Mganga wa zamu katika Kituo cha Afya Kibiti, Dk Sadock Bandiko alithibitisha kuuwawa kwa viongozi hao wa kijiji hicho.

Picha na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi

Leave A Reply