The House of Favourite Newspapers

Wakati Malinzi na Wenzake Wakisota Kortini… Usaili wa Wagombea TFF Waendelea

0

 

IKIWA ni saa chache baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) kwafikisha kortini Kisutu, jijini Dar Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wqenzake ili kujibu tuhuma zinazowakabili usaili wa viongozi wanaowania nafasi za uongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unaendelea kama kawaida.

 

 

Mchujo huo wa viongozi unafanyika katika Ofisi za TFF, Karume jijini Dar es Salaam huku wagombea wawili, Jamal Malinzi aliyekuwa akiwania urais na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ aliyekuwa anawania umakamu Mwenyekiti.

 

 

Uchaguzi umepangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma na Malinzi ndiye anaishikilia nafasi ya Rais wa TFF.

Mbali na Jamal Malinzi, wengine waliofikishwa kortini ni Katibu Mkuu wake Celestine Mwesigwa, Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva, Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ pamoja na anayedaiwa kuwa ni Mhasibu wa Simba ambaye jina lake halijafahamaika.

Live: Hatimaye Yanga Yafungukia Usajili wa Klabu Yake

Leave A Reply