Ijue Siri ya  Jide Kutoboa Miaka 20 Kwenye Game

DAR ES SALAAM: Mwanadada mkongwe kunako Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ amevunja ukimya juu ya suala la kudumu kwenye gemu kwa miaka 20, wasanii kudanga, kulinda hadhi yake, maudhi ya watu na matabaka kwa wasanii wa kike.

Jide amefunguka juu ya uwepo wake kwenye gemu kwa miaka 20, uwepo wa matabaka na uchache wa wasanii wa kike kwenye Bongo Fleva;

 

“Sijaona hayo matabaka na binafsi sina tabaka na mtu.

“Sijawahi kusikia ugomvi kati ya msichana kwa msichana, sanasana bifu huwa nazisikia kwa wanaume, sijasikia bifu la wanawake au labda nipo nyuma nimepitwa.”

 

Jide alieleza siri iliyomfanya alinde hadhi ya kuwa kwenye gemu kwa miaka 20 ni pamoja na kujiepusha na masuala ya uhusiano na mitandao ya kijamii.

“Mimi siigizi maisha, siyo kwamba najaribu kuficha kitu au najitahidi, haya ndiyo maisha yangu, yapo hivi, kuna vitu vingi vinakera kwa sababu kila siku kuna maudhi mapya na wapo ambao wapo kwa ajili ya kuwakera wenzao,” alisema Jide.

 

Aliendelea kusema kuwa hawezi kuingilia maisha ya wanawake ambao wanadanga ili kutoboa katika maisha kwa sababu kila mtu ana namna yake ya kuishi na huwezi kujua ni kitu gani kilichomsababisha mtu kufanya hivyo wala hawezi kumhukumu mtu hata yeye ni binadamu na ana dhambi zake.


Loading...

Toa comment