The House of Favourite Newspapers

Inasikitisha! Baba Amuua Mtoto Wake Wa Miezi Mitano Kisa Kulia Usiku Wa Manane – Majirani Wamlilia – Video

0

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Kubilu Bahege (20) mkazi wa eneo la Kigamboni Mtaa wa Kilimahewa Mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita, anatuhumuwa kumuua mtoto wake wa kiume, Leonard Kubilu mwenye umri wa miezi wa 5, kwa kumpiga kwa kutumia kiatu na mkanda wa suruali kwa madai kwamba alikuwa akilia usiku.

Akisimulia tukio hilo, mama wa mtoto huyo, ameeleza kuwa mumewe alirudi nyumbani usiku akitoka kuangalia mpira ambapo alimpakulia chakula na kuanza kula.

Baada ya muda, mtoto huyo alianza kulia ambapo mwanamke huyo alianza kumbembeleza lakini akawa hanyamazi, jambo lililomfanya mumewe kuanza kumpiga vibao na kumchapa kwa mikanda na alipojaribu kumwokoa mwanae, mwanaume huyo alimng’ata shavu.

 

Leave A Reply