The House of Favourite Newspapers

Isha Mashauzi, Tevez mahaba upya

0

IMG-20150727-WA0012_0 Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’.

Richard BukosPenzi la dhati halifi! Kwa mara ya kwanza tangu ndoa yake ivunjike miaka kadhaa iliyopita, the big boss wa Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’ amenaswa akioneshana mahaba niue hadharani na zilipendwa wake, Jumanne Islam ‘Tevez’.

Tukio hilo lililopigwa chabo na Ijumaa Wikienda lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo Kundi la Mashauzi Classic lilikuwa likizindua wimbo wake mpya uliokwenda kwa jina la Jiamini.

IMG_7476

Katika shughuli hiyo, Tevez aliwasili ukumbini hapo na kumkuta Isha akiwa amepozi kona ndipo mdada huyo, akainuka na kwenda ‘kumchumu’ mumewe huyo wa zamani.

Wakati wakifanya yao, paparazi wetu alikuwa akiwafuatilia kwa umakini sambamba na kuwapiga picha za mnato lakini Isha alipomshtukia, aligeuka mbogo na kumchimbia mkwara:

“Jamani hebu tuachieni umbeya wenu huyu ana mtu wake na mimi nina mtu wangu hamtaki hata watu wasisalimiane jamaniii…”
Kwa upande wa Teves alisema hawezi kukumtupa Isha kwani wametoka mbali.

Leave A Reply