The House of Favourite Newspapers

Ishu ya unga… Mr. Blue: nilimwokoa Chid Benz akarudia tena

0

blue (1)Mr. Blue

GABRIEL NG’OSHA

INA Kheri Sameer ama Mr. Blue si geni miongoni mwa mashabiki wengi wa Muziki wa Bongo Fleva. Msanii huyu alijizolea umaarufu miaka ya 2000 akiwa na ngoma kama Mapozi, Blue, Kiss Kiss na nyingine kibao.

Mr. Blue anayebamba kwa sasa na Ngoma ya Mboga Saba aliyomshirikisha Alikiba hivi karibuni alifunguka mengi kuhusiana na maisha yake kimuziki pia akamgusia mkali wa Muziki wa Hip Hop Bongo aliyetoka naye kipindi kimoja, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.

chid beenz (1)Chid Benz

Mahojiano hayo yalifanywa na mtangazaji wa Kipindi cha Playlist kinachoruka kila Jumamosi kupitia Times FM, Omary Tambwe ‘DJ Lil Ommy, tukaona siyo mbaya tukikusogezea kama yalivyo ili angalau usome ambayo hujawahi kuyasoma kuhusu Mr Blue. Fuatilia hapa chini…

DJ Lil Ommy: Unakumbuka nini katika maisha kabla ya ustaa?

Mr Blue: Nilihaso sana kiukweli kuwa Mr Blue ila kwa kuwa nilikuwa na kipaji nikatusua.

DJ Lil Ommy: Unamshukuru nani kwa kukufanya ufike hapo ulipo sasa?

Mr Blue: Namshukuru Mungu, pia nitoe shukrani kwa msanii Abby Skillz kwani ndiye aliyenigundua mimi na Alikiba.

DJ Lil Ommy: Ulianza kupata skendo za mademu ukiwa mdogo sana uliwezaje kuwatongoza hao mabinti?

Mr Blue: Nilikuwa siwatongozi, wengi walikuwa wanazuzuka na ustaa wangu na walikuwa wananifuata. Kiukweli nilikuwa nawapanga sana.

DJ Lil Ommy: Mastaa walikuwa wangapi?

Mr Blue: Siyo wengi sana naomba nisiwataje ila wasio mastaa ni wengi zaidi.

DJ Lil Ommy: Nini ambacho unakijutia katika maisha yako ya ustaa.

Mr Blue: Kutowasikiliza watu wazima, kwani kama ningefanya hivyo ningekuwa mbali sana kimaisha.

DJ Lil Ommy: Nini ambacho unakichukia katika maisha?

Mr Blue: Starehe zisizokuwa na mpango, kwani bangi, sigara na starehe zingine zimeniharibia mambo mengi.

DJ Lil Ommy: Kama bangi umevuta vipi unga (madawa ya kulevya) ulishajaribu?

Mr Blue: Zaidi ya bangi, sigara, pombe na mengine sijawahi kuvuta unga.

DJ Lil Ommy: Ulishawahi kumshauri Chid Benz kuhusu kuacha dawa za kulevya?

Mr Blue: Ndiyo! Huwa nampigia simu na kumwambia huko alikofika ni mbali sana kwani mimi ujanja wangu wote sijawahi kula unga na hata vilevi vingine nilishaviacha kwa sasa nafanya maisha.

DJ Lil Ommy: Kwani Chid alikwambia alianza kuvuta kwa sababu ipi?

Mr Blue: Kikubwa ni msongo wa mawazo wa kazi zake za muziki ndicho ninachofahamu.

DJ Lil Ommy: Unaweza kufafanua zaidi kivipi msongo wa mawazo?

Mr Blue: Wasanii wengi wanapoachwa na menejimenti zao au watu wanaowasaidia huona kama hakuna maisha na hawawezi kufanya kazi ya muziki bila mtu mwingine.

DJ Lil Ommy: Ulimsaidiaje?

Mr Blue: Niliamua kumpeleka studio na kumlipia kufanya ngoma moja ila nilishangaa baadaye kuona amerudia tena.

DJ Lil Ommy: Unajivunia nini kilichotokana na kazi ya muziki?

Mr Blue: Nina nyumba zangu tatu Tabata, moja imekamilika ndiyo ninaishi nyingine bado zinaendelea.

DJ Lil Ommy: Unakumbuka shoo ya kwanza ulilipwa bei gani?

Mr Blue: Ilikuwa ni shoo ya Mwanza na nililipwa Sh.150,000 ila kiukweli kwa wakati huo ilikuwa nyingi sana.

DJ Lil Ommy: Maisha yakoje kwa sasa?

Mr Blue: Nashukuru Mungu nina mke wangu kipenzi na familia yangu, nawapenda.

Leave A Reply