The House of Favourite Newspapers

Italia Yawekwa Karantini Kukwepa Maambukizi ya Corona

0

RAIA takribani milioni 60 nchini Italia wamewekwa karantini hadi Aprili 3 mwaka huu ili kudhibiti maambukizi ya #Coronavirus kusambaa zaidi. Italia inakuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo barani Ulaya.

 

Akihutubia taifa kwa njia ya runinga, Waziri Mkuu Giuseppe Conte amewataka watu wote kubaki nyumbani na watakaolazimika kutoka wameagizwa kuomba kibali maalum.

 

Hadi sasa, watu 463 wamepoteza maisha nchini humo na idadi ya walioambukizwa imefikia 9,172. Nyumba za ibada zitabaki wazi ikiwa watu watakaa kwa umbali wa mita moja huku mikusanyiko ya ubatizo, harusi na msiba ikipigwa marufuku.

 

Aidha, mechi za Ligi Kuu Soka nchini humo (Serie A) na matukio mengine yote ya michezo yamezuiwa hadi mwezi ujao.

 

Leave A Reply