The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Utamaduni Athibitika Kuwa na Corona

0

WAZIRI wa Utamaduni wa Ufaransa, Frank Riester amethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Olivier Veran, Waziri Riester anaendelea vizuri na anapumzika nyumbani kwake.

Hadi sasa wabunge watano wa nchi hiyo wameambukizwa virusi hivyo. Inaelezwa kuwa inawezekana waziri huyo amepata Corona kutoka kwa mmoja wa wabunge hao.

Aidha, inaelezwa kuwa alikutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, siku chache zilizopita. Watu zaidi ya 3,800 wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo ulimwenguni, huku wengine zaidi ya 110,000 wakiwa na maambukizi.

Leave A Reply