The House of Favourite Newspapers

Izzo B aanika undugu wake na Master J

0

Izzoooo.jpgNa BONIPHACE NGUMIJE

MSANII wa Hip Hop Bongo anayeunda Kundi la The Amaizing, Emmanuel Simwenga ‘Izzo B’ amefunguka kuwa ushikaji wake na mkali wa midundo anayemiliki studio ya Mj Records, Joachim Kimaryo ‘Master J’ ulishapitiliza na kuwa undugu.

IMG_2657Akistorisha na safu hii iliyokaa kiburudani, Izzo B alisema kuwa, ameanza kupiga kazi na Master J kuanzia mwaka 2009 na ni yeye aliyempokea jijini Dar akitoka kwao Mbeya kwa ajili ya ‘kuhuso’ kimuziki.

“Ninamheshimu sana Master J, ni mtu wangu wa karibu ambaye naweza kusema ushikaji wetu ulishafika mbali na kuwa undugu maana tunasaidiana kwenye mambo mengi mno, ndani na nje ya kazi,” alisema Izzo.

Leave A Reply