The House of Favourite Newspapers

Jaffo Atoa Siku 45 Mpwapwa

0

UONGOZI wilaya ya Mpwapwa imepewa siku 45 kukamilisha usimikaji wa mabomba na matanki ya kuhifadhi maji safi na salama kwenye vijiji vya Mbugani, Ngh’ambi na Kiegea katika Wilaya ya Mpwapwa.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dk Selemani Jafo, wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia mifumo ikolojia vijijini ulipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais na unatekelezwa katika Wilaya tano nchini ambazo ni Mpwapwa, Mvomero, Kishapu, Simanjiro na Kaskazini – A

Akiwa Wilayani Mpwapwa katika kijiji cha Nghambi Jafo amekasirishwa na kitendo cha mkandarasi wa Kampuni ya Make Engineering kutoka Dar es Salaam kutokamilisha kwa wakati mradi wa uchimbaji wa visima vyenye urefu wa mita 150 na kumuagiza mkandarasi huyo kukamilisha kazi mapema iwezekanavyo.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha huduma zinasogezwa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Leave A Reply