The House of Favourite Newspapers

Jaji Ajitoa Kesi ya Mbowe

0

Jaji kutoka Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi,Jaji Elinaza Luvanda amejitoa kusikikiza kesi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake watatu.

 

Uamuzi wa kujitoa Jaji Luvanda kusikikiza kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021, umetokana na mshtakiwa katika kesi hiyo, Freeman Mbowe kwa niaba ya wenzake kudai hawana imani na Jaji huyo katika kutenda haki dhidi ya kesi yao.

Mbowe ametoa madai hayo leo Jumatatu Septemba 6, 2021 muda mfupi baada ya Jaji Luvanda kutupilia mbali mapingamizi mawili kati ya matatu yaliyowasilishwa mahakamani hapo dhidi ya washtakiwa hao.

Mhe. Jaji Luvanda ametoa maelekezo kuwa jalada la kesi hiyo lipelekwe kwa msajili kwa ajili ya kupangiwa Jaji mwingine.

 

Mbowe na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama ya kutenda kosa na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya ugaidi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi hapo mahakama hiyo itakapopangiwa Jaji mwingine na washtakiwa wataendelea kubaki rumande.

 

Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakikmu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi katika kesi aliyounganishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka jana 2020.

 

Watuhumiwa hao pia wanakabiliwa mashtaka mbalimbali ikiwemo;

1. Kula njama za kutenda ugaidi (kulipua vituo vya mafuta)
2. Kutenda ugaidi kwa kudhuru viongozi wa serikali ikiwemo kusababisha majeraha kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

3. Mbowe anadaiwa kutoa laki 6 kwa ajili ya kufadhili matendo ya Kigaidi.

4. Watuhumiwa wote kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi.

5. Mshtakiwa wa pili anatuhumiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi

6. Mshtakiwa wa kwanza akituhumiwa kumiliki nguo, begi na koti zote za Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

 

 

Mbali na Freeman Mbowe, wanatuhumiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling’wenya.

 

BEI IMESHUKA! Mnada wa BAJAJI Kutikisa Dar Jumamosi Hii

Leave A Reply