The House of Favourite Newspapers

Jamaa Aliyesaidia Kutuliza Vurugu Kijiji Cha Mpeta Kigoma Amwomba Waziri Mkuu Awadie

0
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha mpeta mkoa wa Kigoma, Gerald Ibrahim maarufu “Serikali” akizungumza na waandishi wa habari.

Jamaa ameibuka kutoka katika kijiji cha Mpeta Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma akiwawakilisha wananchi sita wakimuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa awasaidie walipwe fedha zinazodaiwa kuwa Sh.milioni 15, ambazo ni gharama walizotumia kuleta amani katika kijiji hicho kutokana na mapigano ya askari na wananchi yanayodaiwa kutokea Oktoba 16 na 17,2015.

Aidha katika mgogoro huo inadaiwa walifanikisha kupatikana kwa silaha mbili za Jeshi la Polisi (bastola na SMG) ambazo zinadaiwa zilipotea katika mapigano hayo.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na, Gerald Ibrahim maarufu “Serikali” ambaye ni  muwakilishi wa wanakijiji hao na ndiye anayedaiwa aliongoza kupatikana kwa silaha hiyo na kupatikana kwa amani kutokana na mgogoro huo.

Akiendelea kusimulia waandishi wa habari alidai baada ya tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma walikaa kikao ndipo Katibu Tarafa wa Nguruka alimwambia kuwa amepata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa yeye anaweza kusaidia kupatikana kwa hizo silaha, kuzuia ghasia na kuleta amani kutokana na ushawishi alionao kwa wananchi hao.

“Kutokana na ombi hilo alikubali kwani angeliweza kulipwa kutokana na  kufanya kazi hiyo iliyokuwa inadaiwa ingegharimu Sh.Milioni 15 ambayo anadai hawajalipwa chochote hadi sasa.

Katika kutaka kufikisha kero yake kutokana na kutokulipwa hadi sasa amemwomba Waziri Mkuu awasaidie walipwe fedha zao kwa sababu watumia gharama zao kufanikisha kuleta amani na kupatikana kwa silaha.

Leave A Reply