The House of Favourite Newspapers

Jamaa Aliyekutwa na Damu Nyeupe Azua Gumzo

0

Köhler anafanya kazi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Cologne nchini Ujerumani, amesema kisa kimoja cha kushanga ni pale ambapo mgonjwa mmoja alikuja akiwa anasumbuliwa na kichefuchefu, alikuwa akitapika huku akiugulia maumivu ya kichwa.

 

Mgonjwa huyo mwanaume aliyekuwa na umri wa miaka 39 alikuwa anaumwa ugonjwa wa kisukari, lakini katika siku zilizotangulia alikuwa ameacha kumeza dawa zake.

 

Kulingana na ripoti kuhusu kisa hiki, iliyochapishwa wiki hii katika jarida la masuala ya tiba – Annals of Internal Medicine, mwanaume huyo alipelekwa kwenye kitengo cha dharura, ambako vipimo vilionesha kuwa damu yake ilikuwa nzito kiasi cha kushindwa kuzunguka mwilini inayofahamika kama “Hyperviscosity syndrome inayosababishwa na kupanda kwa viwango vya juu vya mafuta kupindukia katika damu -Triglycerides.”

 

Triglycerides ni aina ya mafuta ya mwilini yatokanayo na vyakula tunavyokula kama vile siagi, na mafuta mengine tunayotumia kupikia vyakula, ingawa viwango vyake vya juu kutokana na sababu nyingine, kama vile, matatizo ya maumbile ya kurithi, unene wa kupindukia, baadhi ya dawa, unywaji wa pombe kupindukia na uvutaji wa sigara.

 

Tiba mbadala

Katika hali kama hii, madaktari hutumia mashine ya kukamua mafuta kutoka kwa damu na hivyo kupunguza uzito wake. Hatahivyo hali ya mwanaume huyo ilikuwa ni ya kupindukia kiasi kwamba vichujio vya kuchuja mafuta vilikwama kwenye mafuta na kuziba.

 

Madaktari waliamua kuchukua hatua haraka ya kuondoa mafuta ya ziada, kurejesha rangi ya damu na hivyo kurejesha hali ya mgonjwa kuwa thabiti.

 

Alipoona mchakato wa kawaida wa matibabu umeshindwa kupata ufanisi, Köhler na timu yake ya madaktari waliamua kufanya tiba inayoitwa phlebotomy, ambayo ni ya kuvuta damu yake yote mwilini na kumuwekea damu kutoka kwa mtu mwingine.

 

“Hatukuwa na la kufanya jingine,” anasema Köhler. “Tulihitaji kumleta mgonjwa katika hali ambayo matibabu ya kawaida ya kuondoa mafuta kutoka kwenye damu ungewezekana tena.” Mbinu hii ilifanikiwa na wakaweza kushusha viwango vya mafuta kwenye damu.

 

“Kwa uelewa wetu, hili ni tukio la kwanza baya zaidi la mgonjwa kuwa na mafuta ya kupindukia kwenye damu kuwahi kushuhudiwa ambalo lilihitaji kufanyiwa mchakato wa kuvuta damu yake yote mwilini na kumpatia damu ya mtu mwingine ili kunusuru mgonjwa baada ya matibabu ya kawaida kutokuwa na ufanisi,” anasema Köhler.

 

Damu ya maziwa
Mojawapo ya mambo yaliyowashangaza madaktari zaidi ilikuwa ni rangi ya damu ya mgonjwa. Madaktari walilazimika kuondoa mafuta kwenye damu.

 

“Mwanzoni rangi ilikuwa imepauka kuliko rangi ya kawaida inayopatikana kwenye mishipa,” anasema Köhler. “Ilikuwa zaidi kama rangi ya mishipa ya ateri lakini ilikuwa nyeupe yenye mng’aro.”

“Baada ya kujichuja, damu nyeupe ikajitenga na damu ya kawaida, ambayo ilijichuja na kubakia chini ya chupa ya kukusanya damu).” Köhler alikiambia kipindi cha Live Science kwamba damu iligeuka na kuchukua “rangi ya maziwa.

Kulingana na dakatari huyo, mwanaume huyo sasa hana dalili za upungufu wa damu residual , na kwa sasa ameruhusiwa kutoka hospitalini na anapokea matibabu nje ya hospitali.

 

Kulingana na daktari Köhler , viwango vya juu vya mafuta katika damu ya mgonjwa vilisababishwa kushindwa kufany akazi kwa sukari ya mwili, unene wa kupindukia, lishe isiyofaa, na ugonjwa wa kisukari ambao haukutibiwa ipasavyo.

Leave A Reply