Jamani faragha siyo usiku tu!

Nianze kwa kuwasabahi na kuwashukuru wasomaji wote wa safu hii pendwa ya XXlove kwa kufuatilia na kutoa maoni kuhusu mada ya wiki mbili zilizopita ya Heshima ni Uwezo Wako wa Faragha. Kiukweli mada hiyo iliwagusa wengi. Nimepokea simu nyingi, ujumbe mfupi wa maneno wa kutosha kuhusu pongezi na ushauri wa mada hiyo.

Napenda kuwakaribisha kwa moyo mkunjufu kwenye mada nyingine nzuri na tamu inayohusiana na masuala hayohayo ya faragha ila kwa mtazamo mwingine. Mada ya wiki hii kama kichwa chake kinavyosema ‘Faragha Siyo Usiku Tu’. Ni muda wowote pale mwenzi wako anapokuhitaji au unapomhitaji.

Utafiti nilioufanya unaonesha kwamba, watu wengi wameifanya faragha au wanaamini ni ya wakati wa usiku tu, kinyume na hapo basi ni anasa au ushamba f’lani, jambo ambalo si kweli.

Faragha ni wakati wowote ule mwenza wako anapokuhitaji au unapomhitaji, iwe asubuhi, mchana wa jua kali, jioni na hata huo usiku, ilimradi mridhiane na kuhamasishana katika kuamsha hali ya ushirikiano mnapoamua kukutana faragha.

Nilizungumza na bibi mtu mzima ambaye huwa namuita kungwi, kuhusu yeye kudumu kwenye uhusiano na mpenzi wake (wengi ni kama babu yetu) alikuwa na haya ya kusema:

“Vijana wa siku hizi, hasa wanawake, hawajui wajibu wao kama wanawake, (alitumia msemo huu, ‘wanawake ni chakula cha wanaume’). Mimi na babu yako alipokuwa anataka kukutana na mimi faragha, hata kama nilikuwa naosha vyombo, nilikuwa naacha nakwenda kumsikiliza mume wangu.

“Hata kama nilikuwa napika, basi nakishusha chungu chini, nakwenda kumsikiliza na hata kumtimizia anachokitaka babu yako. Lakini wasichana wa sasa, usasa umekuwa mwingi, wamegeuza tendo hilo kufanyika usiku tena kwa mazoea na mtindo (staili) uleule, wanaleta ustaa, wanajifanya wasomi hata faragha, hawajishushi mbele ya wapenzi wao, hawataki kujituma, hawataki kuwauliza wapenzi wao nini wawafanyie ili wafurahie wanapokuwa faragha.”

Nimejaribu kuwashirikisha wasomaji wangu maneno ya bibi huyo kwani kila mtu anafahamu kuwa ‘utu uzima dawa’ kwa maana ya kujifunza kitu kutoka kwake na watu wengine waliotutangulia ili kujifunza na kudumisha uhusiano wetu siku zote.

Kwa kawaida, faragha inaweza kuwa sebuleni, jikoni, kwenye kochi, bafuni na kwingineo ilimradi tu mmoja wenu ‘ana shida’ na mwenzi wake kisha kukubaliana, kushirikiana na hatimaye kuzama katika dimbwi zito la mahaba.

Ingawa wakati uko faragha, baadhi ya maeneo niliyotaja lazima yawe yanaruhusu, kama hayaruhusu sana, wakati mwingine mnaweza kubadilisha mazingira kutoka nyumbani na kwenda sehemu nyingine ili tu kubadilisha ladha ya faragha yenu kuwa ya kipekee tofauti na siku nyingine.

Ndiyo kwanza mada hii tamu imeanza. Tukutane wiki ijayo kwa sehemu ya pili. Pia usikose kutembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Mtandao wa Facebook kujifunza mengi kuhusu elimu ya mapenzi.

 

 


Loading...

Toa comment