The House of Favourite Newspapers

JB: Bado Nitapungua Hadi Wanikimbie

0

STAA wa sinema za Kibongo ambaye alikuwa pande la mtu, lakini kwa sasa amepungua, Jacob Steven ‘JB’ amefunguka kuwa hapo alipopungua ni cha mtoto kwani ana mpango wa kupungua hadi watu wamkimbie.

 

Akistorisha na Amani, JB amesema amepungua kwa sababu kuna filamu inakuja ambayo inamtaka awe mwembamba, hivyo alivyo sasa bado anatakiwa awe mwembamba kabisa kama alivyokuwa zamani ndiyo ataendana nayo.

 

“Yaani mnanishangaa nilivyo sasa, mbona hapa mnene sana! Natakiwa kupungua zaidi ili niweze kufiti kwenye filamu ninayokwenda kucheza maana inatakiwa niwe mwembamba,” alisema JB.

Stori: Mwandishi Wetu, Dar

Leave A Reply