The House of Favourite Newspapers

Jengua Azikwa Makaburi ya Mburahati Dar Leo (Picha +Video)

0
Mwigizaji mkongwe, Muhogo Mchungu (kushoto), akishiriki tukio la maziko.

MASTAA, ndugu na jamaa leo wameungana kuuzika mwili wa aliyekuwa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Mohamed Fungafunga, maarufu kama Jengua.

Jengua alifariki jana nyumbani kwa mwanaye, Mkuranga mkoani Pwani alipokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa leo mchana makaburi ya Mburahati Jijini Dar.

Enzi za uhai wake marehemu alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuigiza vizuri uhusika wa ukatili na kupenda kutamani kutoka kimapenzi na wasichana wenye umri mdogo.

Katika mazishi hayo walifurika wasanii wa tasnia mbalimbali kama vile wanamuziki, waigizaji, wanasoka, mabondia na wengineo.

 

Mwigizaji Abuu Abulet a.k.a Mzee wa Chalinze akishiriki maziko ya Jengua.
Sehemu ya waombolezaji waliofurika msibani hapo.
Shehe akiswali  baada ya mazishi.

 

Mwigizaji mkongwe, Bi. Mwenda (kulia), na waigizaji wenzake wakiwa msibani Mburahati.
Mwandaaji mkongwe wa filamu, Musa Banzi (kushoto) Evans Moshi akiwa kwenye maziko.
Mwili wa marehemu ukiswaliwa.
Staa wa filamu za kibongo, Irene Uwoya, hivi ndivyo alivyowasili msibani.
Mwigizaji chipukizi anayechipukia Kobero Chapombe (kushoto) akimsikiliza mwimbaji Baikoko, Omari Kivurande.
Waigizaji Hashim Kambi (kushoto) na Mzee Chillo wakipeana pole msibani hapo.
Muwgizaji Mike Sangu akiwaongoza waombolezaji wengine kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu wakati wa kuelekea kaburini.
Mmoja wa waombolezaji akilia kwa uchungu baada ya kuliona jeneza lenye mwili wa marehemu.
Muigizaji Jacob Stephen a.k.a JB akiwa katika hali ya kukata tamaa baada ya kuliona jeneza na msanii mwenzake.
Waombolezaji wakiwa makaburini.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL 

Leave A Reply