The House of Favourite Newspapers

Jerome Boateng Akutwa na Hatia ya Kumshambulia Mpenzi Wake

0

MWANASOKA wa Ujerumani, Jerome Boateng amepatikana na hatia ya kumshambulia mpenzi wake wa zamani, na ameamrishwa kulipa faini ya euro 1.8m (£ 1.5m). Alikanusha kumjeruhi mama wa binti zake mapacha, aliyeitwa Sherin S, wakati wa mabishano kwenye likizo mnamo 2018.

Aliiambia korti huko Munich kwamba beki huyo wa zamani wa Bayern Munich na mshindi wa Kombe la Dunia mwaka wa 2014 alikuwa amempiga ngumi kali, na alipoteza pumzi kwa muda. Katika ushuhuda wake, Boateng alielezea matukio tofautiya kisa hicho. Chini ya sheria za unyanyasaji wa nyumbani za Ujerumani, anaweza kufungwa jela hadi miaka mitano.

 

Kabla ya kesi hiyo, waendesha mashtaka walimshtumu Boateng kwa kusababisha madhara ya kimwili kwa kukusudia, akirusha taa na sanduku dogo la kupoza kwa mwenzi wake wa zamani wakati wa likizo huko Caribbean mnamo Julai 2018.

Akitoa ushahidi kortini, mwanamke huyo alisema Boateng alikuwa amempiga ngumi, alimvuta nywele, alimng’ata kichwani na kumtukana wakati wa ugomvi. Boateng alikiri katika ushuhuda wake kwamba mivutano iliongezeka wakati wa mchezo wa kadi, na kwamba walikuwa wamegombana.

 

Lakini alisema alikuwa mkali na matusi, akimpiga na kumdhuru mdomo. Alipojaribu kumsukuma mbali naye, alianguka. Alisema alikuwa ametupa mto dhidi ya meza, na taa ilikuwa imeanguka sakafuni.

 

Leave A Reply