The House of Favourite Newspapers

Jerry Tegete: Nitaifunga Yanga ila Sitashangilia

0
Washambuliaji wapya ya Maji Maji, Danny Mrwanda (kulia) na Jerry Tegete (kushoto) kwenye wakiwa na jezi za Sokabet.

STRAIKA wa Majimaji, Jerry Tegete, amesema atajitahidi kuhakikisha anaifunga Yanga leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Majimaji, lakini hatashangilia bao atakalofunga.

 

Tegete anayechezea Majimaji inayodhaminiwa na Sokabet, ni straika wa zamani wa Yanga ambayo ilimsajili akiwa kinda wa Taifa Stars iliyokuwa ikifundishwa na Kocha Marcio Maximo.

 

Tegete ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga wakati alipokuwa akiichezea timu hiyo, amesema kuwa anajua mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na presha ya pande zote mbili lakini akasema kama akifunga bao basi hatashangilia.

 

Akizungumza akiwa kambini Peramiho, nje kidogo ya Mji wa Songea ambako timu yake im­eweka kambi kujiandaa na mchezo huo, Tegete alisema: “Nawahesh­imu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na wana historia nzuri ka­tika soka la Tanzania, lakini kuhusu mchezo wa kesho (leo) sisi tuko vizuri na ninaamini tutashinda.

 

“Tumekuwa katika maandalizi makali kwa wiki yote hii, ikitokea nikafunga bao basi sitashangilia kwa kuwa najiamini, kila mchezo naingia kwa ajili ya kuifungia timu yangu.

 

“Pamoja na hivyo, si unajua ku­funga ni sherehe, naweza nikajisa­hau nikashangilia, ikitokea hivyo basi itakuwa ni bahati mbaya.”

 

Kuhusu kukutana na mabeki wa Yanga akiwemo Kelvin Yondan am­baye alikuwa naye Yanga, Tegete alisema: “Kila mechi kwangu ni fainali, mimi huwa sina utani, mechi ni mechi, lazima tuhakikishe tunapata ushindi.”

 

Alisema kikosi cha Yanga bado hakijachanganya kwa kuwa huu ni mwanzo wa ligi, hivyo timu nyingi zinakuwa bado hazijafunguka.

Leave A Reply