The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Droo Kubwa: Ni Mjengo Wa Kisasa, Umeme Ndani

0

WAKATI siku za kuelekea kuchezeshwa kwa droo kubwa ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili zikizidi kukatika, imefahamika kuwa mjengo huo uliojengwa Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ni wa kisasa wenye vyumba vitatu vya kulala, kikiwemo kimoja ambacho ni ‘Master Bed Room’.

Licha ya vyumba hivyo vitatu, ndani ya mjengo huo pia kuna sebule, chumba cha maakuli, jiko na vyoo ndani, kitu ambacho kitamfanya mmiliki wake akiingia, ameingia. Lakini kitu cha kufurahisha zaidi kuhusu nyumba hii ni kwamba mmiliki wake, ambaye atakuwa ni yule atakayeibuka mshindi katika droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, hatakuwa na haja ya kuhangaika kuweka umeme, kwani atakuta umeingizwa tayari kwa matumizi.

JIDE ROCKSTAR4000 KILA MTU KIVYAKE

Meneja Mkuu wa Global Publishers, ambao ndiyo waendeshaji wa bahati nasibu hiyo, Abdallah Mrisho, alisema jana kuwa, ujenzi wote wa nyumba hiyo umekamilika kwa asilimia mia moja na kwamba mshindi, atajiona wazi jinsi maisha yake yatakavyobadilika.

 

“Lengo letu siku zote ni kurejesha faida kidogo tunayopata kwa jamii tunayofanya nayo kazi, ndiyo maana tumeingia gharama kubwa kuijenga nyumba hii iwe ya kisasa, ili mtu atakayebahatika kuipata, abadili kweli maisha yake na hiyo ndiyo kauli mbiu yetu, kubadili maisha ya watu.

 

“Ni nyumba ya kisasa kwa vigezo vyote, vyumba vitatu vya kulala, sebule kubwa, chumba cha chakula, jiko, choo, bafu vyote hivyo vitapatikana ndani ya nyumba, mmiliki wake atakabidhiwa hati ya kiwanja na ataukuta umeme umeingia, kazi yake itakuwa ni kuongeza umeme ili aendelee na huduma hiyo,” alisema Meneja Mrisho.

 

“Tumekamilisha kila kitu, kilichobakia sasa ni kuwaomba wasomaji wa magazeti yetu ya Championi, Ijumaa Wikienda, Amani, Uwazi, Risasi na Ijumaa kukata kuponi zao za mwishomwisho na kuzituma kwetu haraka iwezekanavyo. Kwa wale wa mikoani, kuponi zao wazipeleke kwa wakala wetu ambao wapo kila sehemu nchini.

 

“Kwa wale wa Dar es Salaam wazilete kuponi zao katika ofisi zetu zilizopo Bamaga, Mwenge na wazikabidhi kwa watu maalum wanaozipokea. Huu ni wakati wa kuhakikisha hawakosi nakala zao kwa vile muda umeshaisha. Wiki mbili zilizobaki wahakikishe hakuna mtu anayeziacha kuponi zake bila kuzileta kwetu, kwa sababu huenda ile utakayoiacha nyumbani, ndiyo iliyokuwa ya mshindi,” anasema Mrisho.

Magazeti Ya Tanzania Leo Jumamosi, Septemba 16, 2017

Nyumba hiyo ya kisasa imejengwa Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa na thamani ya mamilioni ya shilingi na itakuwa ni ya pili kutolewa na Global Publishers, kwani katika bahati nasibu ya kwanza iliyofanyika mwaka jana, mjengo wa aina hiyo ulitolewa.

 

Aliyeshinda katika bahati nasibu hiyo ya kwanza alikuwa ni mwanamama mjasiriamali, Nelly Mwangosi mwenyeji wa Iringa ambaye mjengo wake ulijengwa eneo la Salasala, Dar es Salaam.

 

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inafanyika baada ya kuwepo kwa droo ndogo tano zilizochezeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ambako zaidi ya wasomaji 30 wa magazeti ya Championi, Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikienda waliibuka na zawadi za aina mbalimbali zikiwemo pikipiki, televisheni kubwa, simu za kisasa za mikononi, dinner set na ving’amuzi.

Leave A Reply