The House of Favourite Newspapers

Jini Mauti-15

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:
Nyumbani kwao alikuwa yeye na mfanyakazi wa ndani tu, hakukuwa na mtu mwingine. Kweli nikaenda. Akanipokea kwa furaha, mabusu mfululizo, kilichofuata ni kwenda chumbani kwake. Mapigo ya moyo yalinidunda kwa nguvu, niliogopa mno. SASA ENDELEA…

Sikuwahi kufanya kitendo kile alichotaka tukifanye, kila alipokuwa akiugusa mwili wangu, nilitetemeka sana.
“Thomas….”
“Naam.”

“Naomba tufanye siku nyingine.”
“Kwa nini isiwe leo?”
“Sijajiandaa.”

“Hapana! Linaloweza kufanyika leo, lisingoje kesho mpenzi,” aliniambia. Tayari tulibaki kama tulivyozaliwa.
“Thomas.”
“Unasemaje?”

“Naogopa!”
“Usiogope, hautakufa.”
“Ila nitaumia, naomba tufanye siku nyingine.”
“Siwezi kuvumilia mpenzi! Hata mimi sijawahi, leo ndiyo kwanza siku ya kwanza,” aliniambia.

Alionekana kuchanganyikiwa mno, hakutaka kuniacha hivihivi, alichokifanya ni kunilalia kwa juu. Kweli nilianza kusikia maumivu makali chini ya kitovu, maumivu ambayo sikuwahi kuyasikia kabla.

Nilipiga kelele na kuhisi damu ilianza kutoka, Thomas hakuacha, aliendelea kufanya vilevile. Kila nilipomwambia kwamba naumia, aliniambia ningezoea tu, hivyo aliendelea kama kawaida.

“Thomas….” nilimwita jina lake, tayari chozi lilinitoka.
“Subiriiii…” aliniambia huku akiendelea kufanya alichotaka tufanye.
Ghafla, akiwa kwenye hali hiyo nikaanza kumuona akibadilika, akaanza kutetemeka, mwili ukaanza kukakamaa na macho yake kuanza kubadilika rangi na kuwa mekundu.

iliogopa, Thomas alianza kutisha pale kifuani mwangu, nilipoona hivyo, nikamuweka pembeni, mapovu yakaanza kumtoka mdomoni, macho yakabadilika rangi, mboni nyeusi ikatoka na kubaki nyeupe tu.

Aliendelea kutetemeka, akawa kama mtu anayeumwa degedege. Nilimshika na kuliita jina lake lakini aliendelea kuwa vilevile, mapovu yaliongezeka, damu zikaanza kumtoka masikioni, puani na hata kwenye kucha zake.

Kiukweli nilichanganyikiwa mno, sikujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea. Nikaanza kuliita jina lake huku nikilia, sikuamini kilichokuwa kikiendelea. Wala hazikupita dakika nyingi, hapohapo Thomas akatulia, akafariki dunia kitu kilichonichanganya mno.

Nilibaki nikitetemeka tu, sikuamini kile kilichokuwa kimetokea, kufariki dunia kwa Thomas, mbele ya macho yangu tena juu ya kifua changu kulinichanganya mno. Nilibaki kuwa na hofu kubwa, nilijaribu kumwamsha Thomas mahali pale lakini hakutingishika na nilipoyasikiliza mapigo yake ya moyo, yalikuwa yametulia kabisa.

Nikasimama, sikujua kipi nilitakiwa kufanya, nilibaki nikilia lakini nilichokifanya ni kuupiga moyo konde, huo haukuwa muda wa kulia tena, nilitakiwa nifanye kitu ili niweze kuondoka hata kabla wazazi wake hawajafika.

Nikaufungua mlango na kuelekea sebuleni, nilipofika, sikutaka kutulia, nikaondoka zangu kuelekea nyumbani. Njiani, ndipo nilipoanza kulia sana, nilichechemea kwa maumivu makali chini ya kitovu, nilitembea kwa mwendo wa kasi mpaka nilipofika nyumbani.

“Vipi tena?” aliniuliza mama.
“Hakuna kitu,” nilijibu na kuanza kuelekea chumbani.
“Wewe Davina!”
“Abee mama.”
“Kuna nini?”

“Hakuna kitu mama.”
“Mbona unalia.”
“Nani mimi?” niliuliza, sikulijibu swali hilo, nikaingia chumbani.
Nilipofika chumbani, nikakifuata kitanda na kuendelea kulia. Moyo wangu uliniuma mno, sikuamini kama mvulana niliyempenda kwa mapenzi ya dhati, Thomas alikuwa amefariki dunia tena juu ya kifua changu.

Sikujua tatizo lilikuwa ni nini, sikujua kwa nini Mungu aliamua kufanya jambo lile tena juu ya kifua changu, kila nilipojifikiria, nikaona kwamba Mungu alifanya makosa.
Hata usiku wa siku hiyo tulipokutana kwenye uwanja wa wachawi, sikuonekana kuwa na furaha, nilionekana kuwa mnyonge sana, bibi alifahamu kila kitu kilichotokea, akaamua kunifuata.

Je, kilifuatia nini? Usikose mwendelezo wake wiki ijayo.

Comments are closed.