The House of Favourite Newspapers

Jinsi uzito unavyoathiri uzazi kwa mwanamke-3

0

pregnant_2176694b.jpgWiki iliyopita utakumbuka niliishia kwenye kuelezea kwamba mwanamke mnene pia anaweza kuwa na hamu kubwa ya kula na hula sana hadi kunenepa kupita kiasi.

Kila wakati anakuwa ni mtu wa kutafuna. Hali hii ya kuwa na hamu kubwa ya kula inaitwa Bulimia Navosa. Wanawake wenye matatizo haya wanapoteza mzunguko wa hedhi, huwa wagumba na hata wakipata mimba huwa zinatoka.

Ili ufanikiwe ni vema uwe na umbo na uzito wa wastani, epuka unene mkubwa na wembamba kupita kiasi, ushauri mzuri wa uzito na umbile lako utapata kwa daktari wako wa masuala ya

uzazi.

UFANYAJI MAZOEZI NA UZAZI

Mazoezi ni muhimu kwa afya ya mwanadamu, awe mwanaume au mwanamke. Mazoezi yakizidi kwa mwanamke huleta madhara katika mfumo wa uzazi. Mwanamke anayefanya mazoezi sana

mfano mwanariadha hupatwa na matatizo kama kufunga hedhi, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi na kutopevusha mayai ambapo husababisha ugumba.

Chanzo cha matatizo haya kwa mwanamichezo ni kutokuwa na kiwango kizuri cha mafuta

mwilini kinachosaidia kuchagiza uzalishaji wa vichocheo vya mfumo wa uzazi na msongo wa

mawazo kutokana na kufikiria mashindano.

Kwa hiyo, kwa mwanamke mwanamichezo ni rahisi

sana kupata ujauzito, ni pale atakapoamua kupumzika mazoezi magumu kwa muda, mwili utakaa sawa na atashika mimba.

Kwa hiyo pamoja na kwamba mazoezi huzuia kunenepa na kupunguza mwili, katika lengo la

kupata ujauzito ni vema uwasiliane na daktari wako wa masuala ya uzazi kwa ushauri juu ya mazoezi na uzito unaostahili ili upate mimba.

LISHE NA UZAZI

Wengi wanapenda kujua ni vyakula gani vinaimarisha uzazi. Kwa ujumla hakuna chakula maalumu kwa mwanamke ila chakula chenye kiwango kikubwa cha protini husaidia uzazi kwa

mwanaume kwa kuongeza uzalishaji wa mbegu za kiume.

Vyakula vya vitamini mfano matunda na mbogamboga na mbegu za jamiii ya mboga husaidia kurutubisha na kuimarisha uzazi kwa wanaume na wanawake.

Folic Acid ni vitamin ya muhimu sana kwa wanawake, inapatikana kwenye mboga na matunda hasa ndizi mbivu, kazi yake ni kudhibiti watoto wasizaliwe na kasoro hasa tundu mgongoni na

vichwa vikubwa.

USHAURI

Waone madaktari katika hospitali za mikoa na wilaya kwa uchunguzi wa kina.

Leave A Reply