The House of Favourite Newspapers

Joh Makini Awazodoa Mashabiki Wake

0

RAPA maarufu anayewakilisha pande za Weusi, Joh Makini amedai shabiki yake hana nafasi kwenye maisha yake binafsi na hawezi fuata kile shabiki anasema nje ya muziki wake.

 

Joh amedai ukiacha muziki, ana maisha yake binafsi hivyo hawezi amuliwa na shabiki hadi kwenye personal issues kama ambavyo shabiki mwenyewe hatopenda kuingiliwa kwenye mambo yake binafsi.

 

Joh amesema kwenye ishu za muziki yupo tayari kusikiliza ushauri wa shabiki. Hii imekuja baada ya Joh kutumia ukurasa wake wa Instagram akiachia post na caption iliyouliza mashabiki kwa muonekano wake mpya wa Nywele apewe Yes au No?

Leave A Reply