Kartra

Johora, Diarra Wampagawisha Kocha Yanga

KOCHA wa makipa wa Yanga, Razack Siwa amefunguka kuwa anafurahi kufanya kazi na magolikipa wapya ambao wamejiunga na kikosi hicho hivi karibuni.

 

Magolikipa ambao wamejiunga hivi karibuni na Yanga ni Erick Johora na Djigui Diarra ambao wamechukua nafasi za Metacha Mnata na Farouk Shikhalo ambao mikataba yao imeisha.


Akizungumza na Championi Ijumaa, kutoka nchini Morocco, Siwa alisema kuwa ni makipa wazuri na wenye uwezo mkubwa.


“Namshukuru Mungu tumeanza mazoezi salama na makipa ni wazuri, bado ni vijana naamini katika mazoezi ambayo wanafanya watakuwa vizuri zaidi ya walivyo.


“Tunafanya mazoezi mara mbili kwa siku kwa maana ya asubuhi na jioni wakati joto likiwa limepungua.
“Tunawashukuru viongozi wa klabu kwa kutuleta huku Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, ni sehemu nzuri sana.


“Huu muda ambao nimepata kwa ajili ya kukinoa kikosi kwangu mimi nafurahi sana kwani ni makipa ni wazuri wana
vipaji sana,” alisema Siwa.


Toa comment