The House of Favourite Newspapers

Joshua aichukulia poa rekodi ya kuchemsha

0

KUTOKA kuwa beki mwenye uhakika wa nafasi katika kikosi cha Yanga na Taifa Stars, Oscar Joshua sasa ametimiza dakika 540 bila kuichezea klabu yake, lakini mwenyewe amesema wala haina shida.

Karibu misimu miwili mfululizo, Joshua mwenye taaluma ya uandishi wa habari, alikuwa akichezeshwa beki ya kushoto kikosini Yanga na Taifa Stars lakini sasa katika nafasi hiyo yupo Haji Mwinyi.

Hali mbaya kwa Joshua ilianza muda mfupi baada ya Mwinyi kusajiliwa akitokea KMKM ambapo alicheza Kombe la Kagame pia mechi zote tano za Ligi Kuu Bara.

Hata hivyo, Joshua ambaye amekuwa akikosekana hata katika benchi la wachezaji wa akiba, aliliambia Championi Jumamosi kuwa; “Sihofii chochote na nipo tayari kwa lolote ila nitaendelea kupambana, kwani hivyo ndivyo maisha yalivyo.”

Leave A Reply