The House of Favourite Newspapers

JPM Aeleza Alivyomuibua Kijazi – Video

0

RAIS John Magufuli amesema alikosa mtu wa kumteua kuwa katibu mkuu kiongozi baada ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo, Balozi John Kijazi kustaafu mwaka 2017 na hivyo kuamua kumuongezea muda.

 

 

Amefichua hayo Ijumaa Februari 19, 2021 katika ibada ya mazishi ya  Kijazi aliyefariki dunia juzi usiku Februari 17, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

 

Magufuli amesema Kijazi aliyezaliwa mwaka 1956 umri wake wa kustaafu ulifika mwaka 2017 na alilazimika kuendelea kufanya naye kazi kutokana na kukosa mbadala wake.

 

 

“Nilitembelea maeneo mbalimbali ya barabara na nikakutana na wahandisi wa mikoa. Nilitembelea barabara za mkoa wa Dodoma nikaona zinapitika japo ni za vumbi, nikamuuliza Balozi Kijazi kwa nini, akasema anawasimamia vizuri wakandarasi na fedha anazisimamia vizuri.

 

 

“Alizaliwa mwaka 1956 lakini mpaka leo alikuwa bado ni katibu mkuu kiongozi, maana yake ulipofika wakati wa kustaafu mwaka 2017 nikajaribu kuangalia nani wa kuchukua nafasi yake nikakosa.

 

 

“Nikamuongeza miaka miwili nikifikiri ndani ya muda huo nitapata mwingine lakini hadi mwaka 2019 sikupata, nikamuongeza tena miaka mingine miwili, Mungu akasema umezoea kweli akamtumie yeye mwenye.

 

“Kijazi ameondoka hapa duniani kama shujaa, Maalim Seif ameondoka hapa duniani kama shujaa tuwaenzi na kuyaamini mambo yao waliyoyatekeleza hapa duniani kwa mapenzi makubwa.

 

“Familia ya marehemu Kijazi, Mama Kijazi ninakuomba ukaendelee kulisimamia hili ninajua wewe ni muombaji mzuri endelea kumuombea mume wako, watoto mkaendelee kujenga umoja ulioachwa na baba yenu, ndugu na jamaa akiwepo mdogo wake kasimamieni hilo.

 

 

“Nakushukuru Mzee Kikwete kwa kuja, nawashukuru viongozi wote mliohudhuria hapa nakushukuru sana Baba Poroko, Mungu ambariki sana marehemu Kijazi huko aendapko najua na sisi tuko njiani tunakuja, Mungu aibariki familia.” alisema Magufuli.

 

 

Leave A Reply