The House of Favourite Newspapers

JPM Aamuru Airport ya Zamani Kuwa Soko la Machinga Mbeya – Video

RAIS John Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Mbeya kubadilisha matumizi ya uliokuwa uwanja wa ndege wa zamani kuwa eneo maalumu la machinga mkoani humo ili kufanyia biashara lakini pia wajenge kituo cha mabasi ya abiria na kuwekwa huduma muhimu za kibinadamu.

 

Magufuli ametoa uamuzi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ruanda, Nzovwe, jijini Mbeya leo Aprili 26, 2019, na kuagiza wamachinga wasifukuzwe mjini  lakini kuwepo utaratibu maalum wa kuendesha shughuli zao.

 

Akizungumzia kupanua shughuli za uchumi na huduma zake mkoani humo Magufuli alisema:

 

“Watalii wanashindwa kufika huku kwa sababu ya miundombinu mibovu na asilimia kubwa ya watalii duniani wanatumia ndege na ndiyo maana tumenunua ndege mpya nane, kupanua viwanja lakini pia kuweka rada ambayo itasaidia kukuza usafiri wa anga.”

 

Pia alitumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania kuuimarisha muungano kati ya  Tanzania Bara na Visiwani ukiwa umefikisha miaka 55 leo.

 

“Kuungana, hasa kuunganisha nchi zilizo huru sio jambo rahisi,  wapo wenzetu waliojaribu kufanya hivyo lakini wameshindwa na mnapoungana hata shetani mara nyingi hujitaidi kuwatenganisha,” alisema akisisitiza Watanzania kushikamana kwa ajili ya kuijenga nchi yao.

 

VIDEO: MSIKIE HAPA JPM AKIFUNGUKA

Comments are closed.