The House of Favourite Newspapers

JPM Aanika Siri Nzito ya Tarimba, Slaa – Video

0

MGOMBEA urais wa Tanzania kupitia Cham Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho,  John  Magufuli, amewaomba wananchi wa Kinondoni kumchagua mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo, Abbas Tarimba,  na wananchi wa Ukonga kumchagua Jerry Slaa kwani ni vijana wenye uthubutu na wanaweza kumsaidia vyema kutimiza ndoto za kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo hayo.

 

Amesema hayo leo Jumatano, Oktoba 14, katika Viwanja vya Tanganyika Packers wakati akifanya mkutano wake wa kampeni kwa majimbo ya Wilaya ya Kinondoni ambayo ni Kawe na Kinondoni.

 

“Tarimba nimeanza kumjua zaidi alipofiwa na watoto wake wawili ndani ya wiki moja, mmoja rubani na mwingine injinia, nilipokwenda kumpa pole, baba huyu alikuwa anazungumzia tu maendeleo ya Kinondoni, nikamwambia nitafurahi siku moja ukigombea ubunge ukashinda.

 

“Hata mimi makazi yangu ni Kinondoni, Ikulu kule ni Ilala lakini makazi yangu mimi ni Kinondoni. Hata nilipokuwa Waziri wa Ujenzi niliishi Kinondoni, nileteeni Tarimba.

 

“Jerry Slaa baba yake alikufa kwenye helikopta iliyoungua moto wakati akifanya kampeni zangu, na Ukonga wakamnyima kura, kijana amekaa kimya miaka mitano wala hakuhama chama, baba yake amepoteza maisha sababu ya CCM, tumemleta tena kwa wana-Ukonga, nawaomba mniletee Slaa,” amesema Magufuli.

 

Leave A Reply