The House of Favourite Newspapers

JPM Aifumua Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya

0
Rais John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Agosti, 2017 amemteua Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi kuwa Kamishna wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi anachukua nafasi ya Bw. Mihayo Msikela ambaye amerejeshwa Makao Makuu ya Polisi.
Uteuzi wa Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi unaanza mara moja.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Kulevya Bw. Rogers William Siyanga ambaye amemhakikishia kuwa kazi ya kukabiliana na tatizo la biashara na matumizi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri.
Bw. Rogers William Siyanga amesema tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa na ametaja dawa za kulevya ambazo Mamlaka inapambana nazo kuwa ni bangi, heroine, cocaine, kemikali bashirifu na kwamba kwa sasa imeanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.
Amebainisha mikakati mitatu inayotumika katika mapambano dhidi ya tatizo hilo kuwa ni kuzuia dawa za kulevya zisiingie nchini, kutoa elimu kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia dawa za kulevya na kutoa tiba kwa watu walioathirika na dawa za kulevya, na pia ametoa wito kwa watu wenye waathirika wa dawa za kulevya kuwapeleka katika mamlaka hiyo ili watibiwe.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Agosti, 2017
Leave A Reply