The House of Favourite Newspapers

JPM Akabidhiwa Mtambo wa Mawasiliano, Atoa Maagizo Mazito – Video

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 18, 2018 ameshuhudia makabidhiano ya mfumo mpya wa kusimamia uwazi katika mawasiliano nchini (TTMS), Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam ambapo Mkataba kwa ajili ya usimikaji wa mfumo huo ulisainiwa Machi 22, 2013 kati ya SGS na GBG na baada ya kumalizika, ulianza kufanya kazi Oktoba 01, 2013. Mkataba huo wa TTMS ulikuwa wa miezi 60 (miaka 5) na umemaliza muda wake Septemba 20, 2018.

 

“Wakati naingia madarakani, sikuridhishwa sana na utendaji wa taasisi hii, mkataba wa TCRA ulifichwa tukapewa mwingine ambao kipengele cha kukusanya mapato kwenye makampuni ya simu kilikuwa kimefutwa, hakipo. Nilichokifanyacha kwanza ilikuwa ni kumtumbua aliyekuwa Mkurugenzi wa Mkuu wa TCRA, Dkt. Ally Simba na kupeleka Muswada wa Sheria Bungeni haraka, nashukuru Bunge waliingiza kipengele cha kukusanya mapato kwenye makampuni ya simu, leo tunaona matunda yake

 

“Palikuwa na mchezo mbaya sana. Na kweli Tanzania tumeibiwa mno! Hakuna siri. tumechapwa kweli. Tumezoea kweli; Tumia maneno yoyote ya kuonyesha kwamba tumedhulumiwa vya kutosha. angu mfumo huu uanze kufanya kazi, tumeshakusanya bilioni 93.665, bila ya mfumo huu haya mapato tusingeyapata au yangeishia kwa wajanja wachache, pia umesaidia kutambua vifaa vinavyotumika kwenye mitandao na kukusanya mapato stahiki toka kwa watoa huduma.

“TTMS pia itatambua namba za utambulishi yaani IMEI za simu za kiganjani na kuhakikisha vifaa vyote vilivyounganishwa na mitandao ya watoa huduma, vinakidhi viwango vya kimataifa, na kuhakiki mapato yanayotokana na mawasiliano ya simu. Nawapongeza watumishi wote wa TCRA na wote walioshiriki kwenye mfumo huu, nitoe rai msiishie tu kukabidhiwa bali mjijengee uwezo kuhusu mfumo ili yasije kuwakuta wenzenu wa TRA, lakini niwapongeze baada ya kuambiwa kuwa server ya mfumo huu ipo hapa nchini.

 

“Nitoe rai kwa mamlaka ya mawasiliano; kuweni wakali kwa watu wanaotumia vibaya huduma za mawasiliano. Msiwaonee huruma! Wapo waliosema afadhali Mkurugenzi Mkuu (Eng. Kilaba) umemaliza muda wako, sasa ninakuongezea mkataba mwingine wa miaka 5 hapa hapa, uendelee kuitumikia TCRA, Waziri hakikisha unalishughulikia hili haraka. Uzuri bado unaonekana kijana, endelea kuwabana kabisa.

 

“Napenda kurudia agizo langu kwa Taasisi za Serikali kuhakikisha wanatengeneza mifumo ya ukusanyaji mapato, naiagiza BoT kuiunganisha mifumo yote kwenye kwenye Mfumo Mkuu wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji Mapato ya Umma (GePG). Nimearifiwa kuwa kati ya Taasisi 667 zenye kustahili kuunganishwa na Mfumo wa (GePG), 339 tu ndizo zimeunganishwa. Waziri upo hapa, nitashangaa wewe, makatibu wakuu wanaosimamisa taasisi hizo kuendelee kutoziunganisha kwenye mfumo huu huku wakifanya biashara gizani.

 

“Waziri wa Fedha waandikie barua taasisi zote ambazo bado hazijaunganishwa kwenye GePG, nakala moja unipe mimi na nyingine umpe Waziri Mkuu ili niwe nachungulia huko wanachokifanya. Kabla ya kujiunga na mfumo GePG, Shirika la TANESCO lilikuwa likilipia kwa Mawakala wa Kuuza Umeme kiasi cha zaidi ya Tsh. 38 kila mwaka, tangu wamejiunga na GePG sasa hivi hawalipi hata senti moja, wanalipa zero, inamaana wanaokoa Tsh. Bilioni 38 kila mwaka,” amesema Magufuli.

TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.