The House of Favourite Newspapers

JPM Alia na Mauaji ya Watoto Njombe, Atoa Tamko Zito – Video

Rais Dkt. John Magufuli leo Aprili 10, amewahutubia wananchi wa Mkoa wa Njombe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo. Moja kati ya Shughuli anazofanya ni pamoja na uwekaji jiwe la msingi katika Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoani Njombe.

 

“Nilimtimua RPC kwa ajili ya mauaji yaliyokuwa yanatokea hapa Njombe, OCD wa hapa bado yupo? Sasa kuanzia leo nasema naye aondoke haiwezekani waletwe askari kutoka sehemu zingine kufanya operesheni wao wapo tu hapa.

 

”RPC anapotea Mtoto wa kwanza hadi wa 7 wewe bado upo tu, Mbona watoto wako au mke wako hawapotei? Najua OCD yupo na ananilinda, na yeye aondoke. Tumetuma mpaka watu kutoka Dar kuja kufanya oparesheni! Ikitokea tena, RC mpaka Mtendaji wa Kijiji ataondoka’.

 

“Ndugu zangu Wabena na Wakinga msiamini ushirikina. Sijawahi kusaini mtu anyongwe ila kama ikitokea kesi ya mauaji ya mtoto na nikaletewa kusaini basi nitamuomba Malaika wangu aniruhusu nisaini. Mauaji haya yameweka doa mkoani Njombe.

 

“Naomba aje kiongozi wa Dini atuongoze sala ya toba kwa mauaji ya Watoto. Baada ya maombi kufanyika. Hata huyu OCD nimemsamehe abaki hapa asiondoke. Hata mimi nitatoa rambirambi zangu kwa familia zilizopoteza watoto wao katika mauaji haya. Nitatoa Tsh. Milioni 5 kwa familia na nitampatia Mkuu wa Mkoa akaziwasilishe. Sasa niko tayari kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara.

 

“Siku nyingine mauaji yakitokea hapa Njombe RC , DC, RAS mnaondoka na hata kama kuna sijui mwenyekiti wa kijiji, Mwenyekiti na katibu wa CCM mnaondoka wote ili kusudi hali kama hiyo isijitokeze tena.

VIDO: MSIKIE MAGUFULI AKIZUNGUMZA

Comments are closed.