The House of Favourite Newspapers

JPM Amuwashia Moto Mbunge “Acha Kumchongea Mwenzio, Simfukuzi” – Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameataka viongozi kuacha malumbano yasiyo na tija na badala yak kujikita katika kuwahudumia wananchi wao ambao wamewapa dhamana kubwa ya kuwaletea maendeleo.

 

Magufuli amesema hayo leo Ijumaa, Oktoba 5, 2019 wakati akizungumza na wananchi a Songwe mara baada ya uzinduzi wa Barabara ya Mpemba – Isongole iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe na ujenzi wa Hospitali ya tunduma.

 

“Mh Rais kinachosababisha Ileje isiendelee zaidi ni Mkurugenzi wetu kutotoa ushirikiano kwetu amekuwa kikwazo,” amesema Mbunge wa Ileje Janet Mbene.

 

“Sitamtoa Mkurugenzi Ileje hadi nijiridhishe vizuri , viongozi tuache kuchongeana haya ndiyo yanayotukwamisha…. Mkurugenzi na Wizara msimamieni huyu mkandarasi afanye kazi usiku na mchana, ili ajue kuwa pesa za Watanzania sio za mchezo,” amesema Rais Magufuli.

Comments are closed.